Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 3 2 /
M U N G U M W A N A
K I A M B A T I S H O C H A 4 3 Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo Don L. Davis
Utangulizi: Ulimwengu tunaoishi sio ule unaoonekana kuwa halisi, lakini kwa kawaida ni ule ambao sisi au wengine wameutunga ili tuishi ndani yake.
Kuita ‘Kitu Kitu’
Waamuzi watatu kwenye kongamano la waamuzi wakijigamba kila mmoja kwa mwenzake kuhusu umahiri wao kama waamuzi wa ligi kuu: I. M wamuzi wa Kwanza: Wengine huiita mipira na wengine huiita shuti, lakini mimi huiita jinsi ninavyoona! II. M wamuzi wa Pili: Wengine huiita mipira na wengine huita shuti, lakini mimi huiita jinsi ilivyo! III. M wamuzi wa Tatu: Wengine huita mipira na wengine huita shuti, lakini si kitu hadi niite kitu! Ni nini kiini cha safari ya imani ya Ukristo, asili ya theolojia na mafundisho ya Kikristo, moyo wa maadili ya Kikristo, kiini cha tumaini la Kikristo? Ni Yesu Kristo. Yeye ndiye kiini na chimbuko la imani na maisha ya Mkristo. Vili tulivyo, yote tunayoamini, na yote tunayoelewa kwamba Mungu anafanya ulimwenguni yanahusiana na mtu huyu wa kipekee, ambaye pamoja na upekee wake bado mnyenyekevu:
• Ambaye twafahamu kidogo sana kuhusu sura na utu wake • Ambaye hakusafiri maili 200 kutoka mahali alipozaliwa
• Ambaye tuna simulizi chache tu za kuzaliwa na hadithi kuhusu ujana wake • Ambaye hatuambiwi chochote kuhusu miaka ya maisha yake kuanzia umri wa miaka kumi na mbili hadi thelathini, hata na wale waliomwabudu zaidi. • Ambaye alihudumu kwa miaka mitatu tu, na kukataliwa na wenzake, watu wa nchi yake, na taasisi za kidini
Made with FlippingBook - Share PDF online