Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 3 5
M U N G U M W A N A
Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)
• Kwetu sisi tunaoamini, utukufu wa Mungu wenyewe unang’aa katika uso wa Yesu, 2 Kor. 4:6. • Utimilifu wa Uungu, uzuri wa utukufu wa Mungu unaonekana waziwazi zaidi katika utu na kazi ya Yesu Kristo (Kol. 2:9) - Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. E. Ukristo ni Kristo, yaani kuwa na mahusiano na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye tunaamini aliishi, akafa, na kufufuka ili kutuleta katika uhusiano sahihi na Mungu. • Sio maadili na kutenda mema (tunaishi vyema baada ya kukutana na Kristo) • Sio maisha ya familia tu (tunakuwa vile Mungu anataka tuwe baada ya kumjua Kristo) • Sio masomo ya kidini na liturujia (dini zingine zina maadili mema, programu nzuri za ibada, mafundisho ya kujitolea, na vitabu vingi vitakatifu).
Yesu Ndiye Njia Pekee ya Kumwendea Mungu
Msafiri alimchukua mwongozaji wa kumpeleka katika eneo la jangwa. Wawili hao walipofika kwenye ukingo wa jangwa, msafiri, alipotazama mbele, aliona mbele yake mchanga usio na alama za chochote kilichopita hapo, si nyayo za watu wala za wanyama, njia au alama ya aina yoyote. Akamgeukia mwongoza-njia wake na kuuliza kwa sauti ya mshangao, “Njia iko wapi?” Kwa jicho la karipio, kiongozi alijibu, “Mimi ndimi njia.”
Maandiko Yanaelekeza Kwa Kristo
Mara tano katika Agano Jipya Maandiko yanamtaja Yesu kuwa kusudi la kuandikwa kwa Maandiko Matakatifu. Yeye ndiye sababu ya hadithi, iliyogawanywa katika nusu mbili zisizolingana (Mwa. 1:1-3:15, na Mwa. 3:16 - Ufu. 21). Ukitazama sehemu yoyote ya Biblia, utamwona hapo. Kuna nakala ya shaba ya Azimio la Uhuru iliyochongwa moja kwa moja kwenye sleti ya shaba, iliyotengenezwa kwa usahihi wa kina na maelezo ya kupendeza. Ukirudi nyuma kidogo na kulitazama
Made with FlippingBook - Share PDF online