Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 3 6 /
M U N G U M W A N A
Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)
chapisho hilo la Azimio, hata hivyo, unaweza kuona taswira ya George Washington ikitokea kwenye maandishi. Ilifanyika hivyo kwa utiaji kivuli na uchongaji ili kumwonyesha Bw. Washington kupitia chapisho la Azimio. Katika mawazo yangu, Biblia ina kusudi moja kuu – kumfunua Yesu Kristo, ili, kwa imani ndani yake, tupate kufanyika watoto wa Baba! Yote tunayofanya katika TUMI ni kutafuta njia za kutangaza ukuu na uwezo wa Kristo na Kazi yake, na jinsi inavyohusiana na kuwa mfuasi wa mjini na kufanya huduma ya mjini kupitia makanisa ya mijini miongoni mwa maskini. Mamia ya majina, mifano, taswira, na mafumbo katika Maandiko humrejelea Kristo: • Yeye ni Mkate wa uzima – Ule wenye lishe kamili na nguvu • Yeye ni Adamu wa Pili – mkuu wa jamii mpya ya wanadamu • Yeye ndiye Ufufuo na Uzima – Ambaye jina lake pekee linaweza kushinda kifo na uharibifu • Yeye ni Bwana wa wote - mtawala aliyechaguliwa wa Mungu kurejesha utawala wa Mungu • Yeye ni Mfalme wa Amani - Yule ambaye nguvu zake pekee zitarudisha amani katika ulimwengu wetu wenye matatizo. Yesu ndiye ufunguo wa kumwelewa Mwenyezi Mungu na kazi yake.
II. Kisha, Tunaona kwamba Andiko hili Linamfunua Yesu Kama Ukombozi wa Mungu Uliokamilika. Yesu Peke Yake Ndiye Nabii na Kuhani wa Mungu Aliyepakwa Mafuta Kuturudisha Katika Uhusiano na Mungu.
A. Yesu ndiye njia pekee ya kupatanishwa na Mungu; hakuna mtu mwingine au jina lililopo ambalo linaweza kutuleta katika uhusiano mpya na uliokombolewa na Mungu. Angalia tena Wakolosai 1:17-20 - Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni
Made with FlippingBook - Share PDF online