Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 4 /
M U N G U M W A N A
4. Kila ulimi utakiri kwa hiari au bila kupenda kuwa Yesu ni Bwana.
5. Kuinuliwa (viumbe vyote kuinama, kuungama, na kukiri ubwana wa Yesu) kutaleta utukufu na heshima kwa Mungu Baba aliyemwinua Mwana kwa sababu ya dhabihu na utii wake.
III. Ulazima wa Kujifunza Juu ya Kristo katika Huduma na Utume Mjini
Jina la Kristo linaenea kila mahali, linaaminika kila mahali likiabudiwa na mataifa yote yaliyoorodheshwa hapo juu, na linatawala kila mahali. ~ Tertullian (c. 197, W) 3.158. Ibid. uk. 93.
1
A. Shambulio la uongo na upotofu wa kidini: kuna hitaji kubwa la watu wanaoweza kubaini uongo wa kidini wa adui leo na kuukataa kwa ujumbe wa wazi wa wokovu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.
1. 1 Timotheo 4:1-3
2. Kujifunza juu ya Kristo kunaweza kutupatia silaha dhidi ya kuongezeka kwa udanganyifu wa kishetani katika nyakati tulizonazo, Yoh. 8:31-32.
B. Kuchanganyikiwa kwa giza la kiroho: lipo hitaji kubwa la watu wanaoweza kuonyesha namna ambavyo Yesu wa Nazareti amethibitisha tena mamlaka na haki ya Mungu ya kutawala ulimwenguni, na jinsi anavyoweza kuleta ukombozi na ushindi kwa wote wanaomwamini .
1. 2 Timotheo 4:1-5
2. Kujifunza elimu ya Kristo kunaweza kuangusha ngome za adui na kuiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo, 2 Kor. 10:3-5.
Made with FlippingBook - Share PDF online