Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 4 7

M U N G U M W A N A

Yesu na Maskini (muendelezo)

B. Kiti cha Hukumu cha Mfalme, Mt. 25:31-45 Mathayo 25:34-41 - Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake. 1. Makundi mawili ya watu: kondoo na mbuzi 2. Majibumawili:moja kubarikiwa na kukumbatiwa, lingine kuhukumiwa na kukataliwa 3. Hatima mbili: kondoo katika Ufalme wa urithi wao, walioandaliwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu; mbuzi katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake. 4. Miitikio miwili: mmoja alikuwa mkarimu, mwema, mtoaji; mwingine asiyejali, katili, mbinafsi 5. Kundi lile lile la watu: mwenye njaa, mwenye kiu, mgeni, aliye uchi, mgonjwa, mfungwa. 6. Kiwango sawa: kwa jinsi ulivyowatendea kwa wema au kwa ubaya watu hawa, wale walio chini kabisa kimaisha, ulinitendea mimi .

Made with FlippingBook - Share PDF online