Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 4 8 /
M U N G U M W A N A
Yesu na Maskini (muendelezo)
C. Yesu alifanya ionekane kama wale ambao hawakustahili kabisa lakini waliotubu wangekuwa warithi wa Ufalme. Mathayo 21:31 - Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu. Marko 2:15-17 - Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata. 16 Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.
D. Huduma kwa maskini ni huduma kwa Bwana Yesu – alijihusisha nao kikamilifu.
Hitimisho: Moyo na nafsi ya huduma ya Yesu vilielekezwa kwenye mabadiliko na ukombozi wa wale ambao walikuwa hatarini zaidi, waliosahaulika zaidi, waliopuuzwa zaidi. Kama wanafunzi wake, na tutende vivyo hivyo.
Made with FlippingBook - Share PDF online