Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 5 3
M U N G U M W A N A
Kufundisha Mtaala wa Capstone
• Kwanza, soma kwa makini utangulizi wa Moduli unaopatikana katika ukurasa wa 5, na pitia Mwongozo wa Mkufunzi ili kupata kuelewa kile ambacho kitafundishwa katika kozi. Kitabu cha Mwanafunzi kinafanana na Mwongozo wa Mkufunzi. Mwongozo wako, hata hivyo, unakuwa na maelezo na nyenyo zaidi ambazo zinaweza kupatikana katika sehemu ya maelezo ya mwisho iliyopo mwishoni mwa kila somo. Marejeo kutokana na maelekezo haya yameonyeshwa kwa alama katika mstari wa mpaka wa kushoto. Majaribio, mtihani wa mwisho, na jedwali la majibu vyote vinaweza kupatikana katika tovuti ya TUMI satellite gateway . (Hii inapatikana kwenye kwenye satelaiti [matawi] zote zilizothibitishwa). • Pili, unashauriwa sana kutazama mafundisho haya katika DVD zote mbili kabla ya kuanza kozi. • Tatu, unatakiwa usome kila kazi ambayo unapewa inayohusiana na mtaala, iwe vitabu vya kiada, makala au viambatisho. • Nne, inawezakuwanamsaadakupitiamadakuuzakitheolojiazinazohusiana na kozi kwa kutumia kamusi za Biblia, kamusi za kitheolojia, na vitabu vya mafafanuzi ili kuzizoea zaidi mada kuu zinazotakiwa kufundishwa katika mtaala • Tano, tafadhali fahamu kwamba wanafunzi hawapimwi kwa mazoezi ya kujisomea. Haya yanatolewa ili kuwafanya wanafunzi wapate uelewa kamili wa kile ambacho moduli inafundisha, lakini hiyo haimaanishi kwamba inatikwa wanafunzi wawe wasomaji hodari ili kuelewa kile ambacho kinafundishwa. Kwa wale wanaosoma moduli hizi kwa lunga tofauti na kiingereza, vitabu vinavyopaswa kusomwa vinaweza visipatikane katika lugha yako. Tafadhali chagua kitabu kimoja au viwili vinavyopatikana katika lugha yako – vile ambavyo unaamini vinaongelea vizuri sana kile kinachofundishwa katika moduli hii – na uwape hivyo wanafunzi kama mbadala wa hivi vingine. • Mwisho, anza kufikiria kuhusu maswali ya msingi na maeneo ya mafunzo ya huduma ambayo ungependa kujifunza zaidi pamoja na wanafunzi kwa kuzingatia maudhui ambayo yanaenda kufundishwa.
Kabla Kozi Haija Anza
Made with FlippingBook - Share PDF online