Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 5 4 /

M U N G U M W A N A

Kabla ya kila somo, lazima kwanza utazame maudhui yanayotakiwa kufundishwa yanayopatikana kwenye DVD kwa ajili ya kipindi, na kisha tengeneza sehemu ya Kujenga Dalaja na ya Uhusianishaji kwa ajili ya somo hili.

Kabla ya kila somo

Pitia upya Mwongozo wa Mkufunzi ili kuelewa malengo ya somo na ukusanye mawazo kwa ajili ya shughuli za kujenga dalaja zinazowezekana (njia mbili mpaka tatu za kujenga dalaja zinatolewa ambazo unaweza kutumia, lakini uwe huru kujitengenezea za kwako, kama utaona hilo litakusaidia zaidi.) Kisha, tengeneza sehemu ya kujenga dalaja ambayo inawapeleka wanafunzi kwenye maudhui ya somo na kukamata usikivu wao. Kama ilivyo kanuni, njia za kujenga dalaja zinaangukia katika makundi matatu. Vinasa usikivu, zinakamata usikivu wa wanafunzi na kuwapeleka kwenye mada ya somo. Vinasa usikivu, vinaweza kutumiwa vyenyewe katika darasa lenye wanafunzi wenye hasama nzuri au pia vinaweza kuchanganywa na mbinu nyingine kama ambavyo imeelezwa hapa chini. Mifano: • Kuimba uwimbo wa ufunguzi unaohusiana na ujumbe wa somo. • Kuonyesha katuni au kichekesho fulani ambacho kinahusiana na suala linalozungumziwa katika somo. • Kuwaomba wanafunzi wasimame upande wa kushoto wa chumba cha darasa kama wanaamini kwamba ni rahisi kuwafundisha watu namna ya kupata wokovu kwa kutumia vitabu vya Injili na kisha uwaambie wengine wanaoamini kwamba ni rahisi kuwafundisha watu namna ya kupata wokovu kwa kutumia vitabu vya Nyaraka wasimame upande wa kulia. Mbinu za kusimulia hadithi hapa anaweza kuwa mkufunzi ndiye anayesimulia hadithi ambayo inaonyesha umuhimu wa kile kinachoenda kufundishwa katika somo au anaweza kuwaambia wanafunzi wasimuliane yale waliyopitia kuhusiana na mada inayoenda kujadiliwa. Mifano: • Katika somo la kazi za mchungaji, Mkufunzi anaweza kuhadithia hadithi kuhusiana na namna ya kufanya mazishi na akawaambia maswali na changamoto ambazo zilionekana katika tukio hilo.

Kuandaa Sehemu ya Kujenga Dalaja

Made with FlippingBook - Share PDF online