Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 5 6 /

M U N G U M W A N A

na pia inawaandaa kwa baadhi ya vitu ambavyo vitajadiliwa katika sehemu ya Uhusianishaji ambayo inakuja baadae, japokuwa unaweza kutengeneza kauli yako ya mpito kulingana na majibu ya wanafunzi wakati wa sehemu ya Kujenga Dalaja. Ni muhimu wakati wa kupanga ufikirie pia nini kitakachosemwa. Maswali matatu ya msingi kwa ajili ya kufanyia tathmini sehemu ya Kujenga Dalaja ambayo umetengeneza: • Je ina ubunifu na inasisimua? • Je inalenga mahitaji na matarajio ya kundi husika? • Je inawaongoza watu kuelekea kwenye somo na inaibua shauku yao kuhusiana na somo hilo? Kwa mara nyingine, pitia Mwongozo wa Mkufunzi ili kuelewa malengo ya somo na kukusanya mawazo kwa ajili ya shughuli za uhusianishaji zinazofaa kwa maudhui ya somo. Kisha, tengeneza sehemu ya uhusianishaji ambao unasaidia wanafunzi kuunda muunganiko mpya kati ya kweli za somo na maisha (maana halisi) na wajadili mabadiliko mahususi katika namna yao ya kuamini, mtazamo au matendo ambayo yanatakiwa yatokee kama matokeo (kufanyia kazi). Unapopanga, uwe na tahadhari kidogo usitengeneza sehemu ya muunganiko ambao ni mahususi sana. Kwa ujumla sehemu hii ya somo inatikiwa ije kwa wanafunzi kama mwaliko wa ugunduzi wa pamoja kuliko kama zao la matokeo fulani ambayo yalishatarajiwa kabla. Kiini cha kila sehemu ya uhusianishaji ni swali (au mfululizo wa maswali) ambayo yanauliza wanafunzi kwa namna gani kuijua Kweli kutabadilisha kufikiri kwao, mitazamo, na tabia (tumejumuisha na baadhi ya maswali ya sehemu ya uhusianishaji ili “kuwapa hamasa” wanafunzi wako na kuchochea kufikiri kwao, na kuwasaidia kutenegeneza maswali yao wenyewe yanayotokana na hali halisi za maisha yao). Kwa sababu haya ni mafunzo ya kitheolojia na kihuduma, mabadiliko ambayo tunayohitaji zaidi ni yale ambayo yanahusiana na wanafunzi kuwafundisha na kuwaongoza wengine katika muktadha wao wa huduma. Jaribu na lenga katika kuwasaidia wanafunzi kufikiri kuhusu eneo hili la kutendea kazi katika swali ambalo unalitengeneza.

Kuandaa Sehemu ya Uhusianishaji

Made with FlippingBook - Share PDF online