Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 5 7

M U N G U M W A N A

Sehemu ya uhusianishaji inaweza ikatumia mifumo mbalimbli. Wanafunzi wanaweza kujadili maana yake na namna ya kutendea kazi kwa pamoja katika kundi linaloongozwanamkufunzi aukatikamakundimadogomadogowakiwanawanafunzi wengine (inaweza kuwa mjadala wa wazi au ukifuata mfumo fulani wa maswali yaliyoandaliwa kabla). Kutumia uchunguzi kifani pia kwa kawaida ni namna nzuri ya kuanzisha mijadala. Bila kujali njia iliyotumika, katika kipengele hiki mkufunzi na kundi linalojifunza, wote lazima wafanyike chanzo cha hekima. Kwasabau wanafunzi wenyewe tayari ni Viongozi wa Kikristo, huwa kuna utajiri mkubwa wa maarifa na uzoefu ambao unaweza kupatika kutoka kwa wanafunzi wenyewe. Wanafunzi wanatakiwa kushauriwa kujifunza wao kwa wao lakini pia kutoka kwa Mkufunzi. Kanuni kadhaa zinatakiwa kuongoza mijadala ya sehemu ya uhusianishaji unayoiongoza: • Kwanza, lengo la msingi katika sehemu hii ni kuibua maswali ambayo wanafunzi wanayo. Kwa maneno mengine, maswali yanayojitokeza kwa wanafunzi wakati wa somo ndio yanapewa kipaumbele kuliko yale maswali ambayo mkufunzi ameyaandaa kabla – japokuwa maswali yalilotengenezwa na mkufunzi bado yatakuwa nyenzo muhimu sana za kujifunzia. Sambamba na hili ni muhimu kufikiria kwamba swali linaloulizwa na mwanafunzi mmoja mara nyingi ni swali ambalo yumkini linaweza kuwepo kwa kundi zima. • Pili, jaribu kuelekeza mjadala kwenye vitu halisi na mahususi kuliko vile vya kinadharia au kidhahania zaidi. Sehemu hii ya somo imekusudiwa kulenga kwenye hali halisi za maisha ambazo zinawakumba wanafunzi fulani katika darasa lako. • Tatu, usiwe na hofu kueleza hekima uliyoipata kupitia huduma yako mwenyewe. Wewe ndiwe nyenzo kuu kwa wanafunzi na hivyo wanategemea kwamba yale masomo ambayo umejifunza na wao watayapata pia. Hata hivyo,siku zote weka akilini kwamba tofauti ya tamaduni, muktadha, na haiba zinaweza kufanya kile ambacho kilifanya kazi kwako, kisifanye kazi marazote kwa kila mmoja. Tengeneza mapendekezo, lakini jadili na wanafunzi kama uzoefu wako unaweza kufanya kazi katika muktadha wao na kama hapana, ni nini kinaweza kurekebishwa ili ufanye kazi na kwao pia.

Made with FlippingBook - Share PDF online