Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 5 9

M U N G U M W A N A

Kutumia Vipengele vya Video Kila somo lina vipengele viwili vya video, kila video moja ina urefu wa dakika kama 25. Baada ya kufundisha sehemu ya kujenga dalaja (ikijumuisha kauli ya mpito), onyesha kipengele cha kwanza cha video kwa ajili ya wanafunzi. Wanafunzi wanaweza kuendelea kujifunza na kuandika yale wanayojifunza kutumia Kitabu cha Mwanafunzi ambacho kina muhtasari wa kile kinacho onyeshwa katika marejeo ya Maandiko na nyenzo nyingine ambazo zinatumiwa na yule mzungumzaji kama marejeo. Baada ya kuwa sehemu ya kwanza imetazamwa, ongea na wanafunzi kuthibitisha kama kweli kile kilichoonyeshwa kimaeeleweka. Kuthibitisha kama kile kilichotazamwa kimeeleweka Mwendelezo Kwa kutumia Mwongozo wa Mkufunzi, chunguza ufahamu kwa kuuliza maswali yaliyo orodheshwa katika sehemu ya “Maswali kwa Mwanafunzi na Majibu”. Fafanua kila eneo la uelewa ambalo wanafunzi wameonyesha kutolielewa vizuri kupitia majibu yao. Waulize wanafunzi kama kuna maswali yoyote ambayo wanayo kuhusiana na maudhui kisha myajadili pamoja kama darasa. Zingatia - maswali hapa yanatakiwa yahusu zaidi maudhui yaliyotazamwa na sio namna ya kutendea kazi kile walichojifunza. Maswali kuhusiana na namna ya kutendea kazi yatakuwa ndio shabaha kubwa katika sehemu ya uhusianishaji inayofuata. Mpate mapumziko mafupi kama darasa kisha rudia huu mchakato katika kipengele cha pili cha video.

• Muhtasari wa Dhana Kuu • Kutendea kazi somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi • Uchunguzi Kifani • Marejeo ya Tasnifu ya Somo • Nyenzo na Bibliografia • Kuhusianisha somo na huduma

Fundisha Sehemu ya Uhusianishaji

Made with FlippingBook - Share PDF online