Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 6 3
M U N G U M W A N A
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Alikuja
MAELEZO YA MKUFUNZI 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 1, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alikuja . Lengo la jumla la moduli ya Mungu Mwana ni kuwapa wanafunzi maelezo ya jumla kuhusiana na Yesu wa Nazareti na kazi yake kwa kuzingatia theolojia (tafakari) juu ya maana ya kunyeyekezwa kwake kwa kule kushuka kwake kutoka katika utukufu na kuinuliwa kwake baada ya kifo chake, ufufuo, kupaa kwake, na kurudi kwake. Msisitizo kupitia mada nne za masomo haya unafanya iwe rahisi kufahamu kiini cha muundo msingi wa moduli hii: Yesu alikuja, aliishi, alikufa, na alifufuka na atarudi. Kanuni ya Imani ya Nikea ni msingi muhimu wa kitheolojia wa masomo haya. Yote yametungwa ili kukuwezesha kurudi pamoja na wanafunzi wako kwenye muhtasari huu wa msingi wa Imani, na ni hili ndilo unalopaswa kuzingatia. Jambo moja lazima lisisitizwe tangu mwanzo. Ukweli katika moduli hii unaeleweka hata kwa wasiojua kusoma na kuandika na wasio na elimu, lakini hawapaswi kukubali uvivu au uzembe. Utahitaji kuwasaidia wanafunzi wako kushughulisha akili zao kuhusiana na kweli zilizomo katika moduli hii na maana za baadhi ya maarifa ambayo ni ya kidhahania zaidi, ukiwapatia changamoto ya kutumia akili zao kadiri inavyowezekana, paispo kukubaliana na jaribu la kusema kwamba maarifa haya hayana umuhimu kwa huduma ya mijini au sio muhimu kwa maisha yao binafsi. Kitu ambacho wao kama viongozi wa mijini lazima wawe nacho ni ufahamu kamili, wa kina, na mpana juu ya Yesu Kristo na kazi yake, na hakuna njia ya kuujua ukweli huu wa kibiblia bila juhudi, kujidhabihu, na uwekezaji. Ondoa mawazo yote ya mwanafunzi yeyote anayeamini kuwa kuna njia za mkato za mchakato huu; maarifa ya Kristo yanadai mwitikio wetu kuhusu Kweli uwe makini, wenye nidhamu; kadhalika ndivyo tunavyopaswa kuitikia kwa habari ya ukengeufu na uzushi, na uongo ambao unalenga kuondoa ukweli. Jukumu lako litakuwa kuwasaidia kuelewa umuhimu wa kufikiri kwa bidii; kama Maandiko hapa chini yanavyoonyesha, huu ni wajibu wetu kama viongozi na walezi wa viongozi: 2 Timotheo 2:15 - Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli. 2 Petro 1:10 - Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. 2 Petro 3:14 - Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
1 Ukurasa 15 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online