Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 6 4 /

M U N G U M W A N A

Wakumbushe wanafunzi wako kwamba moduli hii itakuwa ngumu kuelewa, lakini watabarikiwa sana na matokeo yake. Wewe na wanafunzi wako mtahitaji kumwomba Bwana hekima ambayo ni Roho wake pekee anayeweza kuitoa, lakini Mungu anatuhakikishia kwamba hekima hii inapatikana kwa yule aliye na imani (Yakobo 1:5). Pia angalia malengo yaliyopo hapa tangu mwanzo. Haya hutumika kama miongozo yako, vielelezo na ramani ya barabara ili kutoa dira katika mawazo yako na majadala. Kumbuka, pia, kwamba malengo haya yameelezwa kwa uwazi, hutangulia maudhui ya mafundisho au uwasilishaji wowote, na yametolewa ili uweze kuyasisitiza katika somo lote na wakati wa uwasilishaji na mazungumzo na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo utakavyo tengeneza uwezekano mkubwa zaidi wa wao kuelewa na kufahamu ukubwa na unyeti wa malengo haya. Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi cha darasa. Vuta usikivu wa wanafunzi kwenye malengo ya somo, kwani, kwa maana halisi, hiki ndicho kiini cha lengo lako la kielimu kwa kila kipindi cha darasa katika somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kuwaelekeza kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuangazia haya kila mara, ili kuyaimarisha na kuyasisitiza tena na tena kadri unavyoendelea. Kadhalika, kutokana na aina za maarifa ambayo tutashughulika nayo katika moduli hii ya Mungu Mwana, itakuwa muhimu sana kwako kama mkufunzi na mshauri kurudi kwenye malengo, hata katikati ya mjadala wa somo na uchambuzi wa kina unaoufanya na wanafunzi wako kwenye maudhui. Malengo ya somo si tu kipengele cha utangulizi, bali ni kanuni za kiutendaji ambazo unapaswa kuzirudia tena na tena katika kipindi kizima cha darasa. Kuwa mbunifu kwa hili: ziweke kwenye ubao wa bango, zitengenezee kibendera, ziandike ubaoni au kwenye ubao mweupe, yagawe kwa kila mwanafunzi na uwaite mbele katikati ya kipindi cha somo ili wayarudie mbele ya darasa – tafuta njia mpya na za kuvutia za kuyapa malengo haya umuhimu mkubwa katika ufahamu wa wanafunzi. Hili litaleta faida kubwa.

 2 Ukurasa 15 Malengo ya Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online