Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 6 5
M U N G U M W A N A
Ibada hii imejikita zaidi katika nguvu ya mawazo ya kweli ya Kikristolojia na matokeo yake katika maisha na moyo wa mfuasi wa kweli wa Yesu. Kilicho muhimu sana kwako kusisitiza katika somo hili lote ni kwamba nia yetu kuu ya kujifunza ni kuongeza upendo na ibada yetu kwa Bwana Yesu. Ibada ya Kristo hutangulia na kuunda kazi kwa ajili ya Kristo; tulizaliwa mara ya pili ili kumsifu, kumwabudu Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, na ibada hii inalenga kuwasaidia kuelewa sababu kuu ya kujifunza kwetu habari za Mungu, Mwana. Kusudi letu kuu, shauku yetu iliyo safi, lengo letu kuu ni kuelewa uzuri wake, utukufu wake, na ukuu wake. Tunapofikia kufahamu ubora wa Kristo, wema na asili ya Bwana wetu, tunachochewa kumtii, kumfuata, kumheshimu katika yote tuliyo nayo na tufanyayo. Maandiko yanaonyesha wazi kwamba Mungu Mwenye Enzi Kuu amejifanyia mwenyewe vitu vyote, kutia ndani watu wake, kwa ajili ya ibada na utukufu wake mwenyewe: Zaburi 135:3-6 - Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza. 4 Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa. 5 Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu, Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote. 6 Bwana amefanya kila lililompendeza, Katika mbingu na katika nchi, Katika bahari na katika vilindi vyote.. Zaburi 33:11 - Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi. Kutoka 19:5-6 - Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli. Kumbukumbu 32:9 - Maana, sehemu ya Bwana ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake. Malaki 3:17 - Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.
3 Ukurasa 16 Ukurasa wa 13 Ibada
Made with FlippingBook - Share PDF online