Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 6 6 /

M U N G U M W A N A

Tito 2:14 - ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. Zaburi 115:3 - Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda. Isaya 46:10 - nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. Danieli 4:35 - na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Amosi 4:13 - Kwa maana, angalia, yeye aifanyizaye milima, na kuuumba upepo, na kumwambia mwanadamu mawazo yake, afanyaye asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka; Bwana, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake. Mathayo 28:18 - Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Wakumbushe wanafunzi kwamba kusudi letu la msingi la kusoma fundisho la Kristo si ili kukanusha wazushi au kujadili masuala ya kitheolojia. Badala yake, lengo letu la kwanza ni kukua katika ujuzi wa Kristo ili tumjue, na kwa kumjua, tumpende na kumtii! Uzima wa milele ni kumjua Baba na Yesu Kristo Mwanawe (Yohana 17:3). Yesu ni Bwana na Mungu wetu – hilo lilikuwa ni itikio la Tomaso kwa ushaidi wenye kuthibitika ambao Yesu aliutoa kuthibitisha kwamba hakika yu hai, na kwamba alifufuka katika wafu. Tomaso hakuhitaji kubishana kuhusu theolojia mbele ya Bwana aliyefufuka, bali alithibitisha kusudi la kweli la habari zote za kweli kuhusu Kristo – ibada isiyo na kikomo na kukiri ukuu, utukufu, na uzuri wake unaoakisiwa kwa njia ya utii kwake pasipo masharti. Kadiri tunavyomjua zaidi, ndivyo tunavyompenda na kutaka kumjua zaidi. Kwa hakika ni mduara ulioimarishwa kwa utukufu wa maarifa na upendo na utii unaotutegemeza katika vyote tulivyo na yote tunayofanya. Sisitiza unyeti wa ibada katika masomo yote ya Kristolojia; kazi yetu imejengwa juu yake na inatokana na ufunuo huu wa Kristo kama Bwana mfufuka, unaochanganyikana na upendo na ibada yetu kwake.

Made with FlippingBook - Share PDF online