Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 6 8 /
M U N G U M W A N A
zamani, kutoka siku za kale, na kwamba mfalme atakayekuja ni mzaliwa wa kwanza katika maana ya zama za umielele uliopita. Kilicho muhimu kusisitiza kwa wanafunzi katika sehemu hii ni lugha ya Kanuni ya Imani ya Nikea ya kuwepo kwa Yesu kabla ya kuja kwake duniani katika mwili. Sehemu hii, Muhtasari wa Dhana Muhimu , ni fursa kwako na kwa wanafunzi kupata, kwa njia iliyo wazi na katika mfumo wa orodha, kweli kuu na za kimsingi za mawasilisho ya sehemu zilizopita. Kuelewa dhana hizi muhimu ni muhimu ili kuongeza kina cha ufahamu wa maarifa kibiblia, kitheolojia, kihistoria na yale yatokanayo na Kanuni ya Imani ambayo wanafunzi wako wameshughulika nayo. Kwa hivyo, dhana hizi zinapaswa kupewa nafasi ya umuhimu mkubwa muda unafanya marudio ya matini haya pamoja na wanafunzi, na uzifanye kuwa lengo kuu unapopitia kweli zilizomo na maelezo ya vipindi vya video katika mijadala yako na wanafunzi. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa kwa uwazi na kuzingatiwa kwa uangalifu, kwa faida ya kuwaandaa na majaribio na mitihani, kwani maswali yatatokana moja kwa moja na dhana hizi. Sehemu hii ni muhimu katika kuwawezesha wanafunzi wako kuondoka kwenye hatua ya msingi ya kufanya tu uchanganuzi wa kweli kuhusu jambo hadi kufikia hatua ya kutendea kazi maana za kweli husika, kwa ubunifu zaidi, katika maisha yao wenyewe. Kazi yako katika hatua hii ya somo ni kuwawezesha wanafunzi wako kukabiliana na ukweli wa hali halisi ya maisha yao, na kubainisha masuala muhimu zaidi na yenye faida kwa hatima zao, ambayo yanahusiana moja kwa moja na maswali yao na mambo yanayowahusu. Kwa hivyo, maswali yaliyo hapa chini yanalenga kuwazindua wanafunzi katika uchunguzi wa masuala, mawazo na maswali yao wenyewe. Kilicho muhimu hapa sio kuwataka washughulikie maswali yaliyoandikwa hapa chini, bali kupitia mazungumzo nao upate kuwaongoza katika kukabiliana na masuala, wasiwasi, maswali na mawazo yanayotiririka moja kwa moja kutoka katika na uzoefu wao, na yanayohusiana na maisha na huduma zao. Basi, usisite kutumia muda wa kutosha kujadili swali lolote ambalo huenda likazuka kutokana na tafakuri yao ya maudhui ya video, mazungumzo yao, au hata masuala
7 Ukurasa 38 Muhtasari wa Dhana Muhimu
8 Ukurasa 39 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Mwanafunzi
Made with FlippingBook - Share PDF online