Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 6 9

M U N G U M W A N A

fulani mahususi ambayo yanafaa hasa katika muktadha wa huduma wanazofanya wakati huu. Lengo la sehemu hii ni wewe kuwawezesha kufikiri kwa kina na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na muktadha wa huduma zao. Kwa mara nyingine, maswali yaliyo hapa chini yametolewa kama miongozo na vitangulizi, na hayapaswi kuonekana kama mambo ya lazima. Chagua baadhi ya maswali katika orodha, au uje na maswali ya kwako mwenyewe. Jambo kubwa ni kwamba yajikite katika masuala yenye umuhimu wa sasa, katika muktadha wao na mahitaji yao. Vipengele vya Uchunguzi Kifani katika moduli hii ya Mungu Mwana vimeundwa ili kuwasaidia wanafunzi wako kuunganisha na kuchukua maarifa ya mafundisho na kweli ambazo wamejifunza kupitia masomo haya na kuyatumia katika maisha na huduma zao. Mifano mingi inatokana na hali halisi za maisha katika huduma za mijini ambazo mwandishi amekutana nazo, au anajua wengine ambao wamekutana nazo katika huduma halisi. Hakuna majibu yanayotolewa kuhusiana na maswali yatokanayo na mifano hii, kwa kuwa lengo la mijadala hii ni kuwapa wanafunzi wako “uzoefu wa shambani” katika kukabiliana na matokeo halisi na kweli ya mawazo haya. Wasaidie wanafunzi wako kuchunguza aina mbalimbali zinazowezekana za “majibu sahihi,” na usiwaruhusu kusuluhisha masuala haya haraka au bila kufikiria. Hekima nyingi watakayohitaji katika huduma katika maeneo ya mijini itatokana na uwezo wao wa kutafakari kwa utulivu, kwa uangalifu na kwa kina kweli na masuala yote yanayohusiana na jambo kabla ya kuyafanyia kazi au kuyatolea kauli yoyote Maandiko yanazungumzia mara nyingi aina hii ya “kusubirishwa kwa hitimisho”: Mithali 18:13 - Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake. Kumbukumbu 17:4 - ukiambiwa hayo nawe umeyasikia, ndipo utafute kwa bidii, na tazama, ikiwa ni kweli lina hakika jambo lile, kuwa yafanywa machukizo kama hayo katika Israeli. Isaya 11:3-4 - na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; 4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.

 9 Ukurasa 40 Uchunguzi Kifani

Made with FlippingBook - Share PDF online