Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 7 0 /

M U N G U M W A N A

Yohana 7:24 - Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki. 1 Timotheo 5:19 - Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu. Ayubu 29:16 - Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza. Yohana 7:51 - Je! Torati yetu humhukumu mtu kabla ya kumsikia kwanza, na kujua atendavyo? Tunapaswa kuwasaidia wanafunzi wetu kuwa na ustadi zaidi na zaidi katika kupima habari katika muktadha wa kesi, na kutoa uamuzi wenye ufahamu kulingana na ukweli wa kesi husika na Kweli ya Maandiko. Kipengele muhimu katika ufundishaji wa mtaala wa Capstone ni uchunguzi wa ndani ya nje ya darasa ambao wanafunzi wanaufanya kuhusiana na maarifa ya somo na usomaji wa nyenzo mbalimbali. Hakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa kazi za juma lijalo, hasa Kukariri Maandiko na uandishi wa muhtasari kutokana na kazi za usomaji. Tafadhali, wahakikishie wanafunzi kuhusu asili ya kazi ya usomaji. Hizi hazikusudiwi kuwa ngumu au isiyofurahisha kwao. Badala yake, lengo la kazi za usomaji ni kwamba wasome vitabu hivyo kwa kadiri wawezavyo na kuandika sentensi chache juu ya kile ambacho wanaamini waandishi walimaanisha. Ikiwa wanapata shida kusoma maelekezo ya kazi, basi sisitiza tu “juhudi zao bora” kama kigezo muhimu ambaho kitazingatiwa katika kipindi cha darasa. Bila shaka, kuwa na uwezo wa kuchambua maandishi yaliyoandikwa ni ujuzi muhimu wa kiakili ambao wanafunzi wako wanahitaji kujifunza. Hata hivyo, hatutaki kuwaadhibu au kuwaaibisha wanafunzi ambao viwango vyao vya usomaji vinafanya aina hii ya matini kuwa ya kuogofya au ya kutisha. Kwa hivyo, zaidi ya yote, elezea malengo yako ya kazi ya usomaji kwa namna inayohamasisha kujifunza, na utafute kuwatia moyo katika mchakato huu. Kwa mara nyingine, kwa wale wanafunzi ambao wanaweza kuliona zoezi hili kuwa gumu, wahakikishie kuhusu dhamira ya zoezi hili, na uwasisitizie kwamba uelewa wao wa maarifa yanayowasilishwa darasani ndilo

 10 Ukurasa 43 Kazi

Made with FlippingBook - Share PDF online