Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 7 3
M U N G U M W A N A
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Aliishi
MAELEZO YA MKUFUNZI 2
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa kwa ajili ya Somo la 2, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Aliishi . Katika somo hili tutazangazia masuala kuhusiana na ushuhuda wa Biblia juu ya Umwilisho wa Yesu duniani, kushuka kwake kutoka katika ulimwengu wa utukufu hadi kufanyika mwanadamu ili kuleta wokovu kwa uumbaji na wanadamu. Lengo lako ni kuchunguza kwa kina pamoja na wanafunzi uhalisia wa fundisho la Biblia kuhusu uwepo halisi wa Yesu duniani, kile alichotimiza na maana yake kwetu katika huduma ya mijini. Muhtasari bora wa baadhi ya dhana muhimu zinazohusiana na wazo hili muhimu umetolewa na D. R. W. Wood na I. H. Marshall: Wakati Neno ‘alipofanyika mwili’ uungu wake haukuachwa, au kupunguzwa, au kudhoofishwa, wala hakuacha kutekeleza kazi za kiungu ambazo zilikuwa zake hapo awali. Ni yeye, tunaambiwa, ambaye hutegemeza uwepo wa uumbaji katika utaratibu wake, na ambaye hutoa na kutegemeza uhai wote ( Kol. 1:17; Ebr. 1:3; Yoh. 1:4 ), na kazi hizi kwa hakika hazikusitishwa kwa muda wakati wa uwepo wake duniani. Alipokuja ulimwenguni ‘alijifanya kuwa hana utukufu” kwa nje (Flp. 2:7; Yoh. 17:5), na kwa maana hiyo “akawa maskini” ( 2Kor. 8:9 ), lakini hii haimaanishi hata kidogo kupunguzwa kwa nguvu zake za kiungu, kama vile nadharia zinazoitwa kenosis zinavyo sema. Agano Jipya linasisitiza zaidi kwamba uungu wa Mwana haukupunguzwa kwa sababu ya umwilisho wake. Katika mwanadamu Kristo Yesu, kama asemavyo Paulo, “unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol. 2:9; taz. 1:19). Kufanyika mwili kwa Mwana wa Mungu, hakukuwa kupungua kwa uungu, bali kuchukua asili ya mwanadamu. Sio kwamba Mungu Mwana alikuja kukaa ndani ya mwanadamu, kama ambavyo Roho alifanya baadaye. (Kuutafsiri umwilisho kama “kukaa ndani ya” ndicho kiini cha uzushi wa Unestoria). Badala yake, kilichotokea ni kwamba Mwana katika nafsi alianza kuishi kama mwanadamu kamili. Hakujivika tu mwili wa mwanadamu, akichukua nafasi ya nafsi yake, kama Apollinaris alivyosisitiza; alijitwalia nafsi ya mwanadamu pamoja na mwili wa mwanadamu, yaani aliingia katika maisha ya kiakili ya mwanadamu na vilevile maisha ya kimwili ya mwanadamu. Ubinadamu wake ulikuwa umekamilika; akawa “mwanadamu Kristo Yesu” ( 1 Tim. 2:5; taz. Gal. 4:4; Ebr. 2:14, 17 ). Na ubinadamu wake ni wa kudumu. Ingawa sasa ameinuliwa, “anaendelea kuwa, Mungu na mwanadamu katika asili mbili tofauti, na mtu mmoja, milele” (Westminster Shorter Catechism, Q. 21; cf. Ebr. 7:24 ). ~ D. R. W. Wood and I. Howard Marshall. New Bible Dictionary . (3rd ed.) (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996.
1 Ukurasa 47 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online