Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 7 4 /
M U N G U M W A N A
Kwa hiyo, kwa habari ya kushuka kwake kuja duniani, hatutaki kusisitiza kwa namna yoyote ile kwamba inawezekana kweli alibadilisha asili yake kwa maana ya kupunguza uungu wake , bali alichukua namna ya mwanadamu , yaani, alishiriki nasi asili yetu ya kibinadamu. Haya ndiyo mambo ya kufurahisha nafsi zetu na mioyo yetu, na sio tu kuzaja taarifa katika vichwa na akili zetu. Kumbuka, kusudi halisi la elimu sahihi ya Kristo ni kutuongoza kumpenda Bwana Yesu zaidi na zaidi (Flp. 3:7-8), na sio tu kukidhi shauku ya udadisi wetu juu ya mada dhahania za kitheolojia. Tunashiriki katika somo hili ili kumjua kwa hakika yule tunayempenda na kumwabudu (Yohana 4:24). Tafadhali, tumia muda wako kupitia tena malengo ya somo na kuona namna ambavyo kweli hizi zimeelezwa kwa uwazi. Kama kawaida, jukumu lako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa mijadala na muda wote unapokaa na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo haya katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyotengeneza nafasi nzuri na uwezekano mkubwa zaidi wa wanafunzi kuelewa kwa kina ukubwa na unyeti wa malengo haya. Ibada hii inaangazia utambulisho wa Yesu kama utimilifu wa unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi ajaye, mpakwa mafuta wa Mungu ambaye angekuja na kusimamisha utawala wa Mungu duniani. Kitu ambacho ibada hii inatarajiwa kuingiza katika fahamu za wanafunzi ni muujiza wa ajabu ambao Yesu anawakilisha duniani. Masihi amekuja. Mtiwa mafuta wa Mungu aliyetabiriwa kupitia Musa na manabii amefika. Siku ya wokovu na Ufalme imekaribia, na Masihi amekuja, kama jibu la karne nyingi za kungojea wakati mahususi wa kuja kwa Masihi. Sasa tunajua yeye ni nani, na atafanya nini. Hili linalifanya lile tendo la Yesu kutambulisha rasmi kusudi la ujio wake na utumishi wake katika sinagogi siku ile ya Sabato miaka mingi sana iliyopita kuwa tangazo kubwa zaidi ambalo limewahi kutolewa katika kumbukumbu za historia ya wanadamu. Masihi wa Mungu, Mtumishi na Mfalme aliyepakwa mafuta, sasa ameingia ulimwenguni na anathibitisha hapa na pale kwamba Bwana Yehova analitimiza Neno lake. Kwa hiyo, tukizingatia kwamba Ufalme wa Mungu una pande mbili (yaani “upo tayari/bado haujaja), kinachohitajika hapa ni kuangazia zaidi upande wa Ufalme wa Mungu ambao umekwishatokea kupitia Yesu Kristo. Kama kisemavyo kichwa cha
2 Ukurasa 48 Ibada
Made with FlippingBook - Share PDF online