Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 7 5
M U N G U M W A N A
kazi bora sana ya uandishi ya George Eldon Ladd kuhusu Ufalme, Yesu wa Nazareti anawakilisha Uwepo waWakati Ujao . Katika yeye, maisha ya Enzi Ijayo yalidhihirishwa wazi wazi mbele ya watu wa Israeli. Mafundisho yake, namna alivyotoa pepo, miujiza yake, tabia yake na utu wake—yote haya yanatupa picha ya wazi ya ahadi ya ufalme ambayo Mungu aliwapa baba zao kupitia manabii (Ebr. 1:1-2). Katika mjadala wako wa wazo la ibada usisite kuchochea ndani ya wanafunzi drama na ajabu ya kuja kwa Kristo na kile ilichomaanisha wakati huo na sasa kuhusu uaminifu wa agano la Mungu, na matarajio ya wokovu ulio mbele yetu. Ahadi halisi ya Mungu inatimizwa katika nafsi ya Yesu, na Ufalme wa Mungu sasa unaendelea ndani yake. Mfumo huu wa ulimwengu uliopotoka unapitilia mbali, na siku ya utawala wa Mungu inatimizwa! Tazama baadhi ya maandiko yanayozungumzia ukweli huu: 1 Yohana 2:17 - Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 1 Wakorintho 7:31 - Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita. 1 Petro 4:7 - Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. Warumi 13:12 - Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. Wafilipi 4:5 - Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Waebrania 10:25 - wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia. Yakobo 5:8 - Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia. 2 Petro 3:9-11 - Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe
Made with FlippingBook - Share PDF online