Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 7 6 /
M U N G U M W A N A
vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa. 1 Yohana 2:18 - Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Kwa kuja kwa Yesu Kristo ulimwenguni, zile siku za mwisho zimefika. Ufalme umekuja, na ukamilifu wake hauko mbali sana. Tujiandae kwa sherehe tukufu inayokuja. Katika somo hili lote tutaonyesha namna ambavyo Adamu na Yesu wanafanana na kutofautiana kama wakuu na wawakilishi wa vizazi vya wanadamu, Adamu akiwalisha uzao wa wanadamu uliolaaniwa, na Yesu kama mwakilishi wa uzao mpya uliokombolewa kwa damu yake, na kuhifadhiwa ili kuishi milele pamoja naye katika mbingu mpya na nchi mpya, atakapofanya vitu vyote kuwa vipya. Kilicho wazi katika mjadala wa Umwilisho ni dhana muhimu ya Yesu kubeba sura ya Mungu kama Mwanawe , lakini pia kuwa mwakilishi kamili wa wanadamu mbele ya Baba. Alexander na Rosner wanaelezea tofauti iliyomo katika fundisho hili muhimu katika makala yao kuhusu asili ya Yesu kuwa na sura ya Mungu, na uhusiano kati ya kweli hiyo na Adamu: Jambo lililo wazi katika haya yote ni kwamba Yesu ana sura ya Mungu na ni Mwanawe. Kuna tofauti kati ya sura ya Mungu iliyobebwa na Adamu, ambayo pia inabebwa na wanadamu wote, na sura ya Mungu iliyobebwa na Kristo (2Kor. 4:4; Kol. 1:15) ambayo waamini wanafananishwa nayo (2 Kor. 3:18) ; Kol. 3.10). Usuli wa wazo la mfano wa Mungu katika Kristo (k.m. katika Ebr. 1:3) labda unapatikana katika maelezo ya Hekima kama mfano wa wema wa Mungu (Hekima ya Sulemani 7:26). Kwa hiyo Yesu ni mfano halisi wa Mungu; ikiwa Mungu asiyeonekana angeonekana, angefanana na Yesu. Kwa hiyo Yesu ni mwana wa Mungu, aliye kwa mfano wake, kama vile Adamu alivyokuwa baba wa mwanawe ‘katika sura yake, kwa mfano wake’ (Mwa. 5:3). Paulo hatumii neno ‘Mwana’ mara nyingi sana kwa habari ya Yesu (Rum. 1:3-4; 1 Kor. 1:9; Gal. 2:20; na kadhalika.), lakini kwa kufanya hivyo anaonyesha ukaribu wa Yesu kwa Mungu, na zaidi ya yote ukuu wa dhabihu aliyoitoa Baba kwa kumtoa Mwanawe
3 Ukurasa 52 Muhtasari wa Sehemu ya 1
Made with FlippingBook - Share PDF online