Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 7 7
M U N G U M W A N A
mwenyewe (kama vile Ibrahimu na Isaka; taz. Mwa. 22:2, 12, 16) hadi kufa kwa ajili yetu sote (Rum 8:32). ~ T. D. Alexander and B. S. Rosner. New Dictionary of Biblical Theology . (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001. Tunachotafuta kuwasaidia wanafunzi wetu kuelewa ni kwamba Yesu kwa kweli yuko katika kila njia kama sisi, lakini, wakati huo huo, anawakilisha kielelezo cha mwanzo mpya kabisa kwa wanadamu, yeye ni mzaliwa wa kwanza wa uumbaji. cf. Kol. 1:15-19), malimbuko ya wale walalao usingizi (rej. 1Kor. 15), na mfano halisi wa kwanza wa jamii mpya ya wanadamu ambayo itafanywa kwa mfano wa nafsi yake (Flp. 3:20-21). Tabia sahihi ya asili yake ya kibinadamu, kwa hiyo, inapaswa kuwa ya manufaa kwa kila mtu anayeamini kwamba tutashiriki utukufu wake na kufananishwa na sura yake wakati wa kurudi kwake (1 Yoh. 3:1-3; Rum. 8:29). Katika maswali yaliyo hapa chini utaona lengo ni kufahamu kwa kina maarifa na kweli zinazohusiana na uungu na ubinadamu wa Kristo yaliyoangaziwa katika sehemu yetu ya kwanza ya video. Maelezo yaliyomo katika kitabu cha kazi cha mwanafunzi juu ya kenosis ni njia ya moja kwa moja na yenye ufanisi ya kusisitiza masuala yanayozunguka Umwilisho wa Kristo ulimwenguni, na, nini hasa ilikuwa asili ya unyenyekevu wake alipokuwa duniani. Hakikisha kwamba unachukua muda kuangazia kwa uangalifu na kwa kina dhana muhimu zinazohusiana na Umwilisho wa Kristo, ukizingatia hasa masuala yaliyoangaziwa katika sehemu ya video iliyotangulia. Bila shaka, kama kawaida, hakikisha kwamba unatazama muda wako vizuri hapa na uweze kupitia maswali yaliyo hapa chini na yale yaliyoulizwa na wanafunzi wako. Kuwa makini na mambo yoyote ambayo yanaweza kukuondoa kwenye kusudi la msingi la kupitia kweli za msingi na vidokezo kuu vya somo. Wakati ambapo ni lazima na muhimu kwa somo la Kristolojia kuangazia uzushi hatari na mgumu zaidi kuhusu Kristo, ni jambo lililo wazi sana kwamba hii ni mojawapo ya elimu ngumu zaidi kufundisha. Hili halipaswi kututisha, kwa sababu kadhaa. Uzushi wenyewe ulitokea katika mazingira ambayo ungeaminika zaidi na kuonekana kuwa na uwezekano wa kuaminika zaidi kuliko leo. Pili, mawazo mengi
4 Ukurasa 65 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
5 Ukurasa 65 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Share PDF online