Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 7 8 /

M U N G U M W A N A

ya uongo, kwetu sisi watu wa nyakati za leo, yanaonekana kama “kujisumbua kwa mambo yasiyo na mantiki,” na hayana chembe ya ugumu kwetu kama ilivyokuwa kwao. Na mwisho, mafundisho haya ya uzushi, katika hali yake ya asili, tunaweza kusema yamepoteza ushawishi wake. Kwa hiyo, kuyapa uzito mkubwa ni kuibua masuala ambayo hayana umuhimu kwetu. Ingawa hii inaweza kuwa kweli, uzushi unaendelea kujithibitisha wenyewe kwa njia mpya katika wakati wetu wa sasa, na uwezo wa kutambua mafundisho ya uongo ya Kikristo ni muhimu leo k​ ama ilivyokuwa wakati wa Mitume na Mababa wa Imani. Nukuu katika somo hili juu ya mafundisho mbalimbali ya uzushi zimetolewa ili uweze kuwafahamisha wanafunzi wako juu ya uongo mkuu unaohusishwa na viwango mbalimbali vya mafundisho juu ya Kristo. Pengine hutakuwa na wakati wa kuchunguza uzushi huu zaidi, lakini kwa wale wanafunzi wanaotamani kuuchunguza kwa kina zaidi, kuna kitabu ambacho ni cha uhakika sana kwa faida ya utafiti wao. Kitabu hiki kinaitwa Heresies: Heresy and Orthodoxy in the History of the Church cha Harold O. J. Brown (Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1988). Ni moja wapo ya kazi zenye kina na zenye kueleweka zaidi katika kuelezea aina za mafundisho potofu ya Kikristo yaliyojitokeza katika historia ya awali ya Kanisa, na kile ambacho mafundisho haya yanaweza kumaanisha kwetu leo katika kazi yetu kama walimu wa Neno kwa habari ya Kristo na kazi yake. Moja yamambomuhimu yanayoweza kusaidia sana katika kuwafundishawanafunzi juu ya masuala ya elimu ya Kristolojia ni kujua kile ambacho wanatheolojia wa awali kabisa katika Kanisa la Kristo waliamini kuhusu Kristo. Nukuu ifuatayo ni muhtasari mfupi lakini wa kina kabisa wa kanuni kuu za mababa wa kitume juu ya maisha na kazi ya Kristo. Mababa wa kitume wanashiriki na Kanisa zima imani kwamba Mungu mmoja aliyeko na ambaye ni Muumba na Bwana wa vyote, amemtuma ulimwenguni Mwanawe wa pekee Yesu Kristo. . . . Klementi wa Roma anamwelezea Kristo kama Mwana wa Mungu (1 Klem. 36:4), kama mkuu kuliko malaika (1 Klem. 36:2-5, akirejea Ebr. 1) na kama yule aliyenena kupitia Agano la.Kale (1 Klem. 22:1). Klementi anamzungumzia Kristo kama “ fimbo ya enzi ya ukuu wa Mungu ” (1 Klem. 16:2). Muundo wa Utatu unaorejelea Mungu, Bwana Yesu Kristo na Roho Mtakatifu unapatikana katika 1 Klementi 58:2.

 6 Ukurasa 75 Muhtasari wa Dhana Muhimu

Made with FlippingBook - Share PDF online