Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 8 0 /

M U N G U M W A N A

Kilicho muhimu kuhusu muhtasari huu bora wa dhana ya Kristo katika baadhi ya wanafikra na waandishi wa Kikristo wa kale ni jinsi imani yao katika uungu wa Kristo ilivyokuwa makini na yenye kina. Jambo hili linapaswa kuwatia moyo sana wanafunzi wetu kwamba tafakari ya mapema sana juu ya nafsi ya Yesu Kristo ililingana na imani ya Kikristo ya leo – Walimwamini Yesu wa Nazareti kama Mwana wa Kiungu wa Mungu ambaye alidhihirishwa duniani kwa kusudi la kuufunua utukufu wa Mungu na kuleta ukombozi kwa wanadamu. Uchunguzi kifani huu umeundwa ili kuwasaidia wanafunzi kutafakari kwa kina athari mahususi za ubinadamu wa Yesu Kristo katika huduma zao halisi kwa watu katika majiji. Miunganiko ambayo lazima watengeneze kati ya fundisho na vita halisi ya kiroho na haki katika majiji lazima iwe jambo linaloendelea la kimafundisho unalolikumbatia wakati unapitia dhana hizi na wanafunzi wako. Usidhani kwamba watatambua kirahisi tu umuhimu wa fundisho hili kwa maisha yao binafsi au huduma. Ni wajibu wetu kama wakufunzi na waalimu kuwasaidia kufanya miunganiko kati ya yale ambayo Mungu ametufunulia kuhusu Yesu, na kile ambacho ufunuo huo unamaanisha hasa kuhusiana na aina za maisha ambayo Mungu ametuitia tuishi na kazi aambayo ametuita kufanya miongoni mwa maskini wa mijini. Zingatia sana miunganiko ya aina hiyo unapojadili vipengele hivi vya Uchunguzi Kifani na wanafunzi wako. Maombi ni mojawapo ya nguvu kuu katikamafundisho yote, huduma, na kujifunza. Usiyadharau kamwe, na kila mara tafuta kupata muda zaidi wa kuomba pamoja na wanafunzi wako na kuwaombea. Hakuna nafasi ya kutosha hapa kueleza jinsi ambavyo maombi yamewawezesha kwa kiasi kikubwa na kwa nguvu wanafunzi wa kiroho na viongozi watarajiwa kupata uelewa mpya, kubadilishwa katika maisha yao binafsi, na kupenyeza maana ya mafundisho au ufunuo. Maombi yanaleta tofauti kati ya kutumia tu akili na mantiki ya mtu mwenyewe ili kuielewa Kweli, au kujazwa na kuongozwa na Roho wa Mungu ili kuona kile ambacho Mungu anasema katika kifungu au mazingira fulani. Angalia baadhi ya mifano ya kile ambacho Maandiko yanasema kuhusu umuhimu wa upako wa Roho katika kufundisha Neno la Mungu kuhusu Kristo:

 7 Ukurasa 78 Uchunguzi Kifani

 8 Ukurasa 81 Ushauri na Maombi

Made with FlippingBook - Share PDF online