Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 8 8 /
M U N G U M W A N A
masomo yoyote, mwishoni mwa kozi kunakuwa na mambo mengi yanayopaswa kukamilishwa, na wanafunzi wataanza kuhisi shinikizo la kudaiwa kazi kadhaa kwa wakati mmoja. Njia yoyote ambayo unaweza tumia kuwakumbusha juu ya umuhimu wa kujipanga mapema itakuwa ya manufaa kwao, kwamba wanatambua hilo au la. Kwa sababu hii, tunashauri kwamba ufikirie kukata maksi kadhaa kwenye kazi zitakazokusanywa kwa kuchelewa. Hili halifanyiki kwa lengo la kuwaaibisha au kuwadhuru wanafunzi, bali kama fundisho la kuwafanya wafanye maandalizi ya kazi zao mapema, wasije wakalazimika kufanya kazi zao kwa shinikizo dakika za mwisho, na kujinyima fursa ya kufanya kwa ubora na kwa tafakuri ya kina katika mchakato wa kutekeleza kazi zote mbili. Ingawa kiwango cha maksi za kukatwa kinaweza kuwa cha kawaida, utekelezaji wako wa kanuni ulizojiwekea utawasaidia kujifunza kuwa makini, wenye ufanisi na kujali muda wakati wanapoendelea na masomo yao.
Made with FlippingBook - Share PDF online