Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 8 9
M U N G U M W A N A
Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Alifufuka na Atarudi
MAELEZO YA MKUFUNZI 4
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 4, Yesu, Masihi na Bwana wa Wote: Alifufuka na Atarudi . Bila shaka fundisho muhimu zaidi katika imani yote ya Kikristo ni ufufuo. Ujumla wa Imani na maisha yote ya Kikristo unajengwa juu Kweli hii kuu, kwamba Bwana wetu Yesu yu hai, kwamba kaburi ni tupu, kwamba Shetani, dhambi, na kifo vimeshindwa kupitia kifo chake msalabani. Kwa kweli, ikiwa ufufuo si wa kweli, Ukristo unaweza kuwa udanganyifu mkuu zaidi kuwahi kufanywa juu ya jamii ya wananadamu. Bruce Demarest katika kitabu chetu cha kiada Jesus Christ: The God-Man, kwa ufasaha kabisa anathibitisha kile ambacho Wakristo katika enzi zote wamekuwa tayari kuishi na kufa kwa ajili yake: Katika karne zote watu wamejaribu kuwaheshimu mashujaa wao kwa kujenga minara ya kifahari: piramidi kubwa sana za Misri, zilizojengwa kama mahali pa kupumzishwa kwa ajili mafarao wa Misri; Taj Mahal yenye kumeta-meta, kaburi la mfalme wa Kihindi na mke wake kipenzi; Kaburi la Lenin katika Red Square, mahali ambapo mwili wa kiongozi wa Umaksi umehifadhiwa kwa kufanyiwa mchakato wa uhifadhi fulani wa ajabu; eneo la mazishi katika Mlima Vernon, eneo ulipozikwa mwili wa Rais Washington. Kusema ukweli kabisa, kaburi la Yesu haliwezi kulinganishwa na maeneo haya ya gharama. Lakini kaburi la Yesu linayazidi haya na mengine yote katika jambo moja kubwa na la maana zaidi. Liko tupu! Hayumo! Kiini cha imani ya Kikristo ni ukweli kwamba Yesu Kristo siku ya tatu alifufuka katika wafu na yu hai milele na milele. Kanuni ya Imani ya Mitume inakiri kweli hii kwa maneno rahisi, “Ninasadiki katika Yesu Kristo . . . ambaye. . . siku ya tatu alifufuka katika wafu.” Hakuna dini nyingine ulimwenguni kote ambayo imethubutu kukiri jambo hili kuhusu mwanzilishi wake – iwe Ubudha, Ukonfyushasi, Uislamu, au Umormoni. (Demarest, p. 113). Hakuna somo moja linaloweza kughubikwa na kiburi kiasi cha kutarajia kuelezea kwa undani katika muhtasari wake maajabu ya ufufuo, kupaa, na kurudi kwa Kristo katika utukufu. Kwa sababu hiyo, lengo letu katika somo hili ni kujaribu kuweka katika muhtasari rahisi imani ya kibiblia juu ya mambo hayo, na kisha kuwatia moyo wanafunzi kufanya somo hili kuwa jambo wanalotafuta kujifunza kwa kina katika maisha yao yote . Kwa maana moja, kiini cha tumaini lote la Mkristo kimejumuishwa katika maswali na masuala ambayo somo hili linashughulikia. Adabu na unyenyekevu bila shaka ndio njia bora zaidi ya kushughulika na mafunuo haya makuu na ya ajabu ya ufufuo mtukufu na Ujio Mkuu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Ukurasa 125 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online