Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 9 0 /
M U N G U M W A N A
Eskatolojia ya ufufuo (yaani, mahali pake katika sehemu za mwisho za hadithi ya ulimwengu huu ulioanguka) iko katikati ya maungamo ya mitume. Kwa maneno mengine, ufufuo unaanzisha mlolongo wa matukio yanayohusiana na nyakati za mwisho; ufufuo wenyewe ni alama isiyo na shaka ya eschaton au nyakati za mwisho, iliyowekwa wazi katika mafundisho ya Paulo katika 1 Wakorintho 15. Hapo Paulo anajenga msingi wa Injili yake katika ujumbe uliopokelewa kutoka katika mapokeo ya Kanisa kwamba Kristo alikufa na kufufuka kama yanenavyo Maandiko, na anaithibitisha kweli na ungamo la ufufuo kama fundisho la “umuhimu wa kwanza” (Kiyunani en pro tois , mst. 3; cf. 15:1–11). Kristo alifufuka katika wafu na sasa yu hai “kama yanenavyo Maandiko (15:3–4),” na katika mwanga wa utimilifu wa Ufalme uliorekodiwa katika Maandiko, ufufuo wa Yesu ni utimilifu wa ahadi na kielelezo cha mambo yajayo kwa waamini. Ufufuo wa Yesu ni mwanzo wa mavuno makubwa ambayo waamini wote watashiriki. Hii ndio sababu katika 15:12–34 Paulo anaonyesha jinsi matokeo yangekuwa mabaya ikiwa ufufuo ungethibitishwa kuwa uongo. Ushahidi mzima wa mitume kuhusu Kristo ungekuwa uongo, Imani isingekuwa na maana—ingekuwa kama kushika hewa, waamini ambao tayari wamekufa wangepotea, na kati ya watu wote duniani sisi tungekuwa wenye huzuni zaidi Ni lazima tuelewe msingi wetu wa kweli zilizomo katika somo hili katika mwanga wa kweli hizi kuu. Kama viongozi wa Kikristo watendaji wanaoibukia, wanafunzi wetu lazima waelewe kwamba bila kujali ukweli mwingine wowote, ikiwa hawajatayarishwa kuelewa na kukumbatia Kweli ya ufufuo wa Kristo, kupaa na kurudi kwake, bado hawajajiandaa vizuri au wanakosa sifa ya kumwakilisha Kristo na Ufalme wake mijini. Bila kuelewa na kudhihirisha katika maisha yao maana ya ufufuo na kurudi kwa Kristo, watapoteza msingi wote wa kibiblia, wa kimaadili, na wa kiroho wa kufanya huduma. Ni kweli kabisa kusema kwamba hatuna uchaguzi zaidi ya mambo haya mawili: au tunamwakilisha Bwana aliyefufuka au hatumwakilisha hata kidogo . Acha uzito wa ukweli huu ulainishe moyo na fahamu wako unapojitayarisha kuwaongoza wanafunzi wako katika uthibitisho muhimu zaidi kuwahi kufanywa kuhusu mtu yeyote katika historia ya mwanadamu. Malengo ya somo yametolewa kwa uwazi, na kama kawaida, wajibu wako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi katika kipindi chote cha somo, hasa wakati wa majadiliano na kukaa kwako na wanafunzi. Jiwekee nidhamu hasa katika somo hili ili kuzingatia malengo
Made with FlippingBook - Share PDF online