Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 9 1

M U N G U M W A N A

yaliyotolewa hapa. Upana wa matini haya unaweza kusababisha ukavutwa kwa urahisi kwenye mambo mengi nje ya malengo ikiwa hutakuwa mwangalifu kuhakikisha unajikita zaidi katika masuala muhimu yaliyomo katika na malengo.

Ibada hii inaangazia maisha ya mkristo ambaye maisha yake yamejawa kabisa na kutawaliwa na maono na hadithi ya Bwana. Lengo la hadithi ya Kikristo ni utekaji kamili wa akili na ufahamu – tunatafuta kutekwa na kudhibitiwa kwa kila jambo na maono ya ushindi wa Kikristo kupitia ufufuo wa Kristo kiasi ambacho shauku zetu, vipaumbele vyetu, na matendo yetu yote yataunganishwa katika maono hayo. Kristo Yesu aliingia ulimwenguni, akaikamilisha kazi ya Baba, na sasa amefufuka na kupaa juu. Hivi punde atarudi ili kukamilisha kazi yake katika ulimwengu huu, akiugeuza kuwa milki ya Mungu chini ya utawala wake. “Maono Yenye Heri” kama Wakatoliki wanavyodokeza, ufunuo huu wa Mungu na Mwanawe, na tumaini la mbingu mpya na nchi mpya vinapaswa kuwa kama damu na mapigo ya moyo ya tumaini la mkristo. Taswira na matamanio haya lazima vifanyike kiini hasa cha mapenzi yetu na shauku zetu. Angalia jinsi baadhi ya maandiko ya Agano Jipya yanavyozungumza kuhusiana na jambo hili: Wakolosai 3:1-4 - Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. 1 Yohana 2:15-17 - Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. Warumi 8:5-6 - Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.

 2 Ukurasa 125 Ibada

Made with FlippingBook - Share PDF online