Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
2 9 2 /
M U N G U M W A N A
Luka 12:15 - Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Mathayo 6:19-21 - Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; 20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. Luka 12:33 - Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, mahali pasipokaribia mwivi, wala nondo haharibu. Waebrania 10:34 - Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika vifungo, tena mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu, mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. Yakobo 2:5 - Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao? 1 Petro 1:4 - tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. Mkristo ni mtu ambaye maono yake yamejengwa juu ya vitu asivyoweza kuona wala kuhisi na juu ya hazina za milele ambazo hazina uhusiano wowote na mfumo wa sasa wa ulimwengu, ambao umehukumiwa na ni wa muda. Mkristo mwenye ufanisi zaidi na wa vitendo zaidi ni yule ambaye maisha yake yameundwa na kudumishwa na tumaini ambalo halina uhusiano wowote na mfumo huu wa ulimwengu uliopotoka na ulioangamizwa. Uwezo huu wa kuishi kwa kile kisichoonekana wala kuhisiwa ndicho kiini cha imani ya kweli, ambayo bila hiyo hakuna mtu anayeweza kumpendeza Mungu (Ebr. 11:6). Tumeitwa kwenye maono ambayo hatuwezi kuyaona (ni kinaya iliyoje!), mtazamo utawalao na mtazamo ulimwengu ambao umejikita katika ufufuo wa Kristo. Paulo anazungumzia hili katika Warumi: Warumi 8:23-25 - Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu. 24 Kwa maana tuliokolewa kwa taraja;
Made with FlippingBook - Share PDF online