Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 2 9 3

M U N G U M W A N A

lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana, hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho? 25 Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi. Maono yanayotawala ambayo tunaishi kwayo yanatokana na tumaini ambalo halionekani lakini ni halisi na hakika. Mungu atujaalie tuwe na moyo wa kujiwekea hazina mahali palipotengwa mbali na wizi, kutu na uozo wa mfumo huu wa sasa. Mifano ya rejea au mijadala na vivuta usikivu vifuatayo vinalenga katika kuwafanya wanafunzi kutafakari kiini cha shauku na tafakuri ya mkristo – tumaini la mwamini kwa maana ya kile tunachokitarajia hivi karibuni kama matokeo ya ufufuo, kupaa, na kurudi kwa Kristo. Ingawa kusisitiza “masomo yanayohusiana na unabii” kunaweza kuonekana kuwa jambo lisilo na maana au lisilofaa kama inavyofanywa katika makusanyiko mengi ya kiinjili leo, tumaini la imani ya Kikristo ndio ufunguo wa kila nyanja nyingine ya Imani hii – uaminifu kwa Ufalme, kujitoa kwa Kanisa la Kristo, kudhihirisha maisha thabiti kwa kuyaishi maadili ya Kikristo, na mafuta katika injini ya huduma na utume wa Kikristo. Masomo haya yote yanahusiana moja kwa moja na uelewa wetu na uzoefu wa tumaini tulilo nalo katika Kristo, tumaini ambalo hutokeza matendo ya kishujaa, huduma isiyo na ubinafsi, na matarajio ya furaha ya neema ya Mungu itakayofunuliwa hivi karibuni katika Kristo. Kwa vile kiini cha somo hili ni juu ya matumizi ya kina ya kweli za tumaini la Kikristo katika maisha yetu, unaweza kudokeza baadhi ya dhana hizi katika mijadala yako katika vipengele hivi vya mawasiliano. Ingawa wengi huona tumaini la Kikristo kuwa ni mada ya hapa na pale tu ya kuzingatiwa kwa kawaida wakati wa huzuni na maombolezo kwenye ibada ya ukumbusho na mazishi, mtazamo wa mitume ni kwamba huu ni ukiri na ungamo la kila siku; ni maono yenye nguvu ya kujenga maisha ambayo yanasisitiza uhusiano wetu wote na Mungu na wasafiri wenzetu katika Kristo (k.m., Kol. 3:1-4). Tafuta kukuza ari hii ya shauku na matarajio katika somo hili lote.

 3 Ukurasa 128 Mifano ya rejea

Made with FlippingBook - Share PDF online