Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 9 4 /

M U N G U M W A N A

Andiko kuu katika kuthibitisha hoja ya ufufuo wa mwili, na uhakika wa ufufuo wa Kristo ni hoja ya ajabu na endelevu ya Paulo iliyorekodiwa katika 1 Wakorintho 15. P. S. Johnston anatupa muhtasari wa wazi na wa kina kuhusu umuhimu wa dondoo hii katika makala yake juu ya kifo na ufufuo katika imani ya Kikristo: Kwa Paulo, ufufuo wa Kristo ndio msingi wa maisha ya Kikristo katika ulimwengu huu wa sasa na ndio msingi wa tumaini la wakati ujao, kama anavyoeleza kwa kirefu katika 1 Wakorintho 15. Kwanza anathibitisha ukweli wa kihistoria wa ufufuo wa Yesu kwa kutambua kuonekana kwake kwa mamia ya wanafunzi na hatimaye kwa Paulo mwenyewe (mist. 1–10). Kisha anabainisha jinsi ambavyo imani ya ufufuo lilikuwa fundisho la Wakristo wote wa Kanisa la Kwanza na namna ambavyo kutokuamini kweli hii kungeifanya imani ya Kikristo kuwa upuuzi (mist. 11–19). Ikiwa Yesu hakufufuka, basi alikuwa tu Masihi mwingine wa Kiyahudi aliyeshindwa. Lakini ikiwa alifufuka, basi Ufalme mpya wa Mungu umepambazuka. Kisha Paulo analeta upya mada za kawaida za Kiyahudi katika mtazamo wa Kikristo. Kifo kilikuja kupitia kwa Adamu, ufufuo kupitia Kristo, ambaye sasa anatawala mbinguni akiwa amewashinda maadui zake (kipengele bainifu cha Masihi, ingawa maadui hao kwa kawaida walitafsiriwa kama wa kisiasa; mst. 20–28). Hili lapasa kuathiri sana jinsi waamini wanavyoishi (mist. 29–35). Kisha Paulo anaelezea mwendelezo na tofauti kati ya miili ya sasa na ya wakati ujao kwa kutumia mifano kadhaa (mist. 35-49), na anafupisha mjadala huu kwa vivumishi viwili ambavyo ni vigumu kutafsiri kwa ufupi na mara nyingi vimeeleweka vibaya (mst. 42). Tofauti si kati ya mwili/vyenye kuonekana na visiyo na mwili, lakini kati ya miili tofauti; huu wa sasa ( psychikon ), yaani iliyohuishwa na nafsi, na ule wa baadaye ( pneumatikon ), yaani wenye kuhuishwa na roho. Mwili wa nyama na damu unaoharibika unabadilishwa kuwa mwili usioharibika, na hivyo kifo chenyewe kinamezwa (mist. 50-55). Ufufuo wa Kristo ni sampuli ya awali au kielelezo cha hali ya baadaye ya wakristo [msisitizo wangu]. ~ P.S. Johnston. “Death and Resurrection.” New Dictionary of Biblical Theology . T. D. Alexander, ed. (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001. Ni jambo la maana sana kwamba wanafunzi wapate umahiri wa muhtasari na yaliyomo katika kifungu cha 1 Wakorintho 15, kwani andiko hili linatoa moja ya uchambuzi wa wazi zaidi, wa kina zaidi, na wa kusadikisha zaidi wa jukumu na nafasi ya ufufuo katika imani na mafundisho ya Kikristo.

 4 Ukurasa 129 Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook - Share PDF online