Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 2 9 5
M U N G U M W A N A
Robert Stein anatoa mchanganuo muhimu wa ukweli halisi wa ufufuo kama ifuatavyo: Wakati Agano Jipya linatangaza ufufuo wa Yesu Kristo, haimaanishi kwa tendo hili kwamba kuna kitu kilitokea kwa wanafunzi. Hata hiyvo, bila shaka, kuna kitu kiliwatokea. Lakini hata kama kusingekuwa na kitu kilichotokea baadaye kwa wanafunzi, ufufuo bado ungekuwa wa kweli. Tangazo la ufufuo ni hasa — ufufuo wa Yesu Kristo. ~ Robert H. Stein. Jesus the Messiah: A Survey of the Life of Christ . Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996. p. 274. Msingi huu thabiti wa hoja ya ufufuo umeathiri sana kila nyanja ya imani ya Kikristo, hata hivyo, lazima tusadikishwe kuhusu uhalisia na uhakika wa hoja hii kwanza, ndiposa tunaweza kuchunguza matokeo na athari zake juu ya imani, maisha na huduma yetu kwa Mungu. Sehemu hii inaangazia “Kilimanjaro” ya ungamo la kitume la Agano Jipya, kilele cha ukweli ambacho kinabeba tumaini letu na kufanya ujumbe mzima, maadili na utume wa Kikristo kustahili kuaminika. Yesu Kristo amefufuka katika wafu, na kupaa na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, Mwenyezi! Lengo letu katika sehemu hii ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wetu wanaelewa muhtasari wa msingi zaidi wa kweli zinazohusiana na matukio yote mawili, na kwamba wanaelewa matokeo na manufaa yanayohusiana na yote mawili. Kuhusiana na hili basi, ni hitaji la wanafunzi kufahamu kwa upeo makini na wa kina mambo makuu yanayohusiana na matukio haya. Kagua malengo yako ya sehemu hii, na uhakikishe kwamba namna yako ya kuyashughulikia inajumuisha mambo yote muhimu yanayolengwa kama malengo ya sehemu hii. Katika sehemu hii, huwezi kuangazia kwa mapana dhana kuhusu Ujio wa Pili wa Kristo katika utimilifu wake wote mkuu na wa ajabu. Unachopaswa kutafuta ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wako wana ufahamu wa jumla wa muhtasari mpana wa fundisho ambalo limefundishwa katika muhtasari mfupi na wa muhimu kweli wa Kanuni ya Imani ya Nikea iliyoangaziwa katika sehemu hii. Angalia kama
5 Ukurasa 132 Muhtasari wa Kipengele I-B
6 Ukurasa 141 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
7 Ukurasa 152 Muhtasari wa Dhana Muhimu
Made with FlippingBook - Share PDF online