Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

2 9 6 /

M U N G U M W A N A

wanafunzi wanaelewa na kukumbatia “picha kubwa” iliyosisitizwa na kutangazwa katika matamko ya Kanuni ya Imani. Ikiwa muda unaruhusu, tafuta “kufungua” vipengele vingine muhimu sanjari na mawazo na dhana pana. Hata hivyo, kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wamepata mwanga vizuri kuhusu dhana kuu za kurudi kwa Yesu zilizomo katika ungamo la Kanuni ya Imani kwa habari ya Ujio wa Pili wa Kristo. Kwa vile ufufuo, kupaa, na Kuja Mara ya Pili kunachukua nafasi muhimu sana katika imani na utendaji wetu kama Wakristo, itakuwa muhimu, katika vipengele vya uchunguzi kifani, ujitahidi kuwasaidia wanafunzi kuelewa matokeo ya vitendo ya mafundisho haya katika maisha yao. Mojawapo ya misiba mikuu katika mafundisho mengi leo ni kwamba mafundisho yetu yanajenga pengo lisilopitika kati ya kile tunachoamini na kile tunachofanya katika uhalisia. Ni lazima tuwasaidie wanafunzi wetu kujifunza theolojia kwa ajili ya utendaji, na kuelewa utendaji wao kupitia lenzi ya theolojia. Hatutendi kwa yote mawili tunaposhindwa kuunganisha theolojia yetu na utendaji wetu kwa pamoja. Kama Tertullian alivyodokeza, “Maandiko ya Kimungu yana matumizi makubwa sana. Baada ya kutambua maana iliyokusudiwa na kuitendea kazi, yanaimarisha utendaji wa maisha ya kidini katika maeneo yote,” (Bercot, A Dictionary of Early Christian Beliefs , p. 338). Jaribu kusaidia kuziba pengo kati ya mafundisho ya ufufuo, kupaa, na Ujio wa Pili, na matokeo ya vitendo katika maisha na huduma itokanayo na kweli hizo. Kwa kukamilika kwa somo hili, utahitaji sasa kuelekeza mawazo yako kwenye usimamizi wa kazi za kozi hii. Sasa, kazi yako kama mtathmini na msahihishaji itapaswa kuanza kwa bidii. Tafadhali hakikisha kuwa umepokea mapendekezo ya wanafunzi wote kuhusu kazi zao za huduma, kazi za ufafanuzi wa Maandiko na taarifa nyingine kwa pamoja kwani hili litakuwezesha kubainisha jumla ya maksi za mwanafunzi. Kadhalika, hakikisha unatoa maelekezo yaliyo wazi juu ya sera zako kuhusu kazi zitakazokusanywa kwa kuchelewa. Kama ilivyoelezwa hapo awali, usisite kuwaambia wanafunzi kwamba unahifadhi haki ya kukata maksi kwa kila kazi itakayochelewa kukusanywa bila ruhusa, jambo ambalo linaweza kusababisha mabadiliko ya daraja la ufaulu, au kuwaandikia wanafunzi “Haijakamilika” hadi pale kazi zao zitakapokuwa zimekamilika.

 8 Ukurasa 154 Uchunguzi Kifani

 9 Ukurasa 157 Kazi

Made with FlippingBook - Share PDF online