Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
3 4 /
M U N G U M W A N A
D. Uzushi unaohusiana na kuuelewa vibaya uungu wa Yesu Kristo
Nimeonyesha katika Maandiko kwamba hakuna hata mmoja wa wana wa Adamu, katika kweli yote na kwa namna yoyote, aitwaye Mungu, au aitwaye Bwana. Lakini Yesu Mwenyewe katika haki Yake Mwenyewe, tofauti na wanadamu wote waliopata kuishi, ni Mungu, Bwana, Mfalme wa Milele, na Neno Mwenye Mwili.... Yeye ni Bwana Mtakatifu, wa Ajabu, Mshauri, Mzuri wa uso, na Mungu Mwenye Nguvu. ~ Irenaeus (c. 180, E/W) 1.449. Ibid. uk. 95.
1. Uzushi wa Kiebioni (Ebionism) : Kristo si Mungu.
a. Kikundi cha Wakristo Wayahudi waliosema Yesu alikuwa mtu wa kawaida ambaye nguvu za Mungu zilimjia wakati wa ubatizo wake.
1
b. Kristo alikuja juu ya Yesu wakati wa ubatizo, lakini alimwacha baadaye maishani.
c. Yesu hakuwa Mungu, bali mtu wa kawaida ambaye Mungu alimjia wakati fulani wa maisha yake.
d. Ebionism inapuuza mafundisho ya wazi ya Maandiko.
2. Uzushi wa Ario (Arianism) : Kristo si Mungu kamili.
a. Ario (Arius) alikuwa Mwangalizi (kiongozi wa kanisa) huko Aleksandria katika Kanisa la kwanza ambaye alikana uungu wa Yesu.
b. Maoni yake yalilaaniwa kwenye Mtaguso wa Nikea (Baraza lile lile lililotupatia Kanuni ya Imani ya Nikea).
c. Mtazamo wa msingi: Waariani waliamini katika ukweli kwamba Mungu hana mipaka kabisa (absolute transcendence) . (1) Mungu pekee ndiye wa milele; vitu vingine vyote, (pamoja na Neno) vimeumbwa.
Made with FlippingBook - Share PDF online