Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
3 6 /
M U N G U M W A N A
Hitimisho
» Kabla ya Bwana wetu Yesu kuja duniani, aliishi kama mshiriki wa Uungu (Utatu), kama Neno Aliyekuwepo kabla au Logos . » Lugha ya Kanuni ya Imani ya Nikea, kama inavyofafanua na kuangazia maana ya Maandiko, hutusaidia kuelewa asili ya uungu ya Yesu. Inakubaliana na ushuhuda wa Biblia kuhusu Yesu kuwa mwenye hadhi sawa na Mungu katika sifa na vyeo vyake. » Yesu anaonekana kama Mwana mtakatifu wa Mungu, utimilifu wa unabii wa Agano la Kale kuhusu Masihi, na kama Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kupitia maarifa yaliyomo katika sehemu ya pili ya video. Ufahamu sahihi wa uungu wa Yesu Kristo ni ufunguo wa ujasiri na uhakikishowetukatikakumwabuduyeyekamaMfalmenaMwokoziwetu, tumaini letu kwake kama Bwana wa mavuno, na utumishi wetu kwake kama Mfalme wetu. Licha ya mazoea yetu ya kutotilia mkazo fundisho hili kuu katika mafundisho na mahubiri yetu, ni lazima tuwe na uthabiti wa kutafakari kwa makini maana ya mafundisho haya kwa ajili ya ibada na ufuasi wetu leo. Kuwa mwangalifu iwezekanavyo unapotoa majibu yako kwa maswali yafuatayo, na ujenge hoja zako kwa kutumia Maandiko. 1. Neno Logos linapotumiwa kumhusu Yesu Kristo limaana gani? Je, mafundisho haya kuhusu Yesu kama aliyekuwepo tangu awali yanahusiana vipi na ukiri wa Kanuni ya Imani juu ya uungu wa Kristo? 2. Elezea asili ya uhusiano wa Yesu na Mungu Baba kama “Mwana wa pekee wa Mungu.” Je, dhana hii ina tofauti gani na Yesu kama Mwana wa Mungu “aliyeumbwa kwanza”? 3. Kwauelewawako,Kanuni yaImani yaNikea inamaanishanini inapothibitisha kwamba Yesu ni “wa asili ileile ya Baba?” Je, ni kwa jinsi gani dhana hii inatusaidia kuelewa usawa wa Yesu na Mungu katika asili na kiini? 4. Kanuni ya Imani inathibitishaje fundisho la Biblia kuhusu nafasi ya Yesu katika uumbaji? Je, kweli hii inamaanisha nini kuhusiana na njia ambayo Mungu anategemeza ulimwengu leo ? 5. Orodhesha baadhi ya majina na sifa ambazo Maandiko yanafundisha kwamba Yesu anashiriki pamoja na Mungu. Je, hii inatusaidiaje kuuelewa uungu wa Kristo?
1
Sehemu ya 2
Maswali kwa wanafunzi na majibu
Made with FlippingBook - Share PDF online