Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 4 3
M U N G U M W A N A
Ni katika uhusiano gani au suala gani mafundisho haya yanaweza kuleta athari ya haraka juu ya jinsi unavyoelewa wajibu wako kama shahidi wa Kristo katika familia yako, ujirani, kazi, na huduma yako?. Mwombe Mungu Roho Mtakatifu aongeze ufahamu wako wa kweli hizi unapozihusianisha kimahususi na huduma na mahusiano yako katika maisha yako leo. Kipengele muhimu katika ufahamu wako na matumizi ya Kweli ya Biblia ni nafasi ya dua na sala. Unapochunguza kweli hizi kuhusu asili ya nafsi na kazi ya Kristo, utahitaji mara kwa mara na kwa bidii kumwomba Bwana hekima ya kuielewa Kweli yake, na ujasiri wa kutii maana yake katika kila eneo la maisha yako. Zaidi ya hayo, itakuwa muhimu kwako pia kuomba kwamba Mungu Roho Mtakatifu akupe nafasi maalum ya kufundisha na kutumia kweli hizi kwa wale unaowahudumia, na kuwawezesha kufaidika kivitendo kutokana na maarifa yaliyomo. Tafadhali, utiwe moyo na ujisikie huru kumshirikisha mshauri au mwalimu wako, pamoja na wanafunzi wenzako mahitaji mahususi yanayohusiana na maisha yako binafsi na huduma. Mwombe Mungu akuwezeshe wewe na wao, kwa kadri ya maongozi yake, kutumia kweli hizi kuhusu Kristo aliyeinuliwa juu sana na mwenye hadhi, na uwe tayari kuwainua wengine kwa Bwana katika maombi ukizingatia mahitaji haya haya muhimu akilini.
Ushauri na maombi
1
MAZOEZI
Yohana 1:14-18
Kukariri Maandiko
Kazi ya usomaji
Ili kujiandaa kwa ajili ya kipindi, tafadhali tembelea www.tumi.org/books kupata kazi ya usomaji ya wiki ijayo, au muulize Mkufunzi wako.
Uwezo wako wa kunufaika kutokana na vipindi vya darasani unavyoshiriki na wanafunzi wenzako unategemea moja kwa moja kiwango cha nidhamu na umakini katika kujisomea kibinafsi nje ya vipindi vya darasani. Kwa hivyo, tafadhali hakikisha kwamba umetenga muda wa kutosha kusoma kazi zote, kufanya kazi yoyote ya nyumbani, na kukariri maandiko yoyote yanayohusiana na kazi hizo kama zinavyoelekezwa mwishoni mwa kila somo katika moduli hii. Hii ni muhimu hasa kwa kuzingatia kwamba wiki ijayo kutakuwa na jaribio la maswali kuhusu maudhui (yaliyomo kwenye video) ya somo hili . Kwa kuzingatia haya, tafadhali hakikisha kwamba unatumia muda kupitia madokezo yako ya somo na mjadala wa wiki hii, na uzingatie hasa mawazo makuu
Kazi nyingine
ukurasa 270 10
Made with FlippingBook - Share PDF online