Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

4 4 /

M U N G U M W A N A

ya somo. Soma vitabu na maeneo yote uliyoagizwa kusoma, na uandike muhtasari mfupi usiozidi aya moja au mbili kwa kila eneo ulilosoma. Katika muhtasari huu tafadhali andika uelewa wako bora zaidi wa kile unachofikiri kilikuwa jambo kuu katika kila eneo la usomaji. Usijipe shida kujaribu kutoa maelezo mengi; andika tu kile unachoona kuwa jambo kuu linalozungumziwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali leta muhtasari huo darasani wiki ijayo. (Ona “Fomu ya Ripoti ya Usomoja” mwishoni mwa somo hili.) Katika somo hili tumeona jinsi Kanuni ya Imani ya Nikea inavyotoa muhtasari wa wazi na mfupi kwa ajili ya kutupatia ufahamu kuhusu nafsi na kazi ya Yesu Kristo, iliyofafanuliwa katika mielekeo au mitazamo miwili. Kwanza, kunyenyekezwa kwake (yaani, kufanyika kwake mwanadamu na kufa kwake msalabani kwa ajili yetu), na kisha kuinuliwa kwake (kufufuka kwake, kupaa kwake, na tumaini la kurudi kwake katika nguvu). Akija duniani ili kuufunua utukufu wa Mungu na kuukomboa uumbaji, uwepo wa Yesu hapo awali unaonekana katika nafasi yake kama Mungu Mwana, nafsi ya kiungu aliye sawa na Mungu, kama Aliyetarajiwa katika unabii wa Kimasihi wa Agano la Kale, na kisha kama Mwenye mwili, Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Mungu katika umbo la mwanadamu. Katika somo letu linalofuata tutaangazia kwa kina zaidi kusudi la jumla la kuja kwa Yesu duniani: kutufunulia utukufu wa Baba na kutukomboa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani. Kwa kuzingatia ubinadamu wa Yesu, tutazungumzia umoja wa asili ya Yesu ya kiungu na ya kibinadamu, tukimtazama Yesu kama Yule Aliyebatizwa ambaye alijihusisha na taabu na hatari ya wenye dhambi aliokuja kuwaokoa, Mtangaza Ufalme wa Mungu, na Mtumishi wa Yehova Atesekaye.

Kuelekea Somo Linalofuata

1

Made with FlippingBook - Share PDF online