Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 4 7

M U N G U M W A N A

Yesu, Masihi na Bwana wa Wote Aliishi

S O M O L A 2

ukurasa 273  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea kusudi la jumla la kuja kwa Yesu duniani: kutufunulia utukufu wa Baba na kutukomboa kutoka katika dhambi na nguvu za Shetani. • Kuelezea lugha ya Kanuni ya Imani kuhusu ubinadamu wa Yesu, kuchukuliwa kwa mimba yake kwa uweza wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa kwake na Bikira Mariamu. • Kueleza kwa muhtasari makosa mawili maarufu ya kihistoria ambayo yametokea kutokana na ubishi kuhusiana na Yesu kufanyika mwanadamu: Unestoria (Nestorianism) – kwamba Kristo alikuwa watu wawili tofauti , na Ueutikia (Eutychianism) – kwamba Kristo ana asili moja iliyochanganyika . Mitaguso ya Nikea (325) na Chalcedon (381) ilisuluhisha utata huu, ikithibitisha kwamba Yesu alikuwa Mungu kamili na mwanadamu kamili . • Kufanya tathmini na kukanusha makosa yanayohusiana na kutafsiri ubinadamu wa Yesu vibaya: Docetism ambayo ilidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu na Uapolinari (Apollinarianism) ambao ulidai kwamba Yesu hakuwa mwanadamu kamili . • Kuelezea athari za kiutendaji za umoja wa asili ya Yesu ya uungu na ubinadamu, na umuhimuwa ubinadamuwaYesu kwetu: Yesu, Kuhani wetu Mkuu, anaweza kuchukuliana nasi katika mahitaji yetu na kutuwakilisha mbele za Mungu. Kama Adamu wetu wa Pili, tutafananishwa na mfano wake katika kutukuzwa kwetu pamoja naye wakati ujao. • Kutambua na kutoa utetezi wa kibiblia kuhusu dhana ya Yesu kuwa ni Aliyebatizwa ambaye alijihusisha na masaibu na hatari ya wenye dhambi ambao alikuja kuwaokoa. Kadhalika na dhana ya Yesu kama Mtangaza Ufalme wa Mungu – Yesu alithibitisha tena haki ya Mungu ya kutawala juu ya uumbaji, akidhihirisha kupitia nafsi yake, miujiza, uponyaji, na kutoa pepo, kama ishara za ujio wa Ufalme duniani kwa njia ya nafsi yake. • KuchambuanakufunuadhanayaYesukamaMtumishiwaYehovaAtesekaye, akiakisi utume wake wa Kimasihi kwa kule kutangazwa hadharani kwa

Malengo ya Somo

2

Made with FlippingBook - Share PDF online