Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
4 8 /
M U N G U M W A N A
huduma yake. Kadhalika na jinsi Yesu alivyojidhihirisha kuwa Mtumishi wa Yehova aliyetarajiwa kupitia kutangaza kwake Habari Njema kwa maskini, kudhihirisha haki katikati ya watu wa Mungu, na dhabihu yake mbadala kwa niaba ya watu wa Mungu kuwa “fidia kwa ajili ya wengi.”
Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu
Ibada
Luka 4:14-21 - Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando. 15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote. 16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Yesu wa kweli asimame tafadhali! Kama onyesho la zamani la mchezo ambapo washindani walitafuta kudanganya jopo la watu mashuhuri kuhusu jinsi walivyokuwa katika maisha halisi, wakati wa Yesu wengi walikuwa wakicheza mchezo wa kubahatisha kuhusu utambulisho wa kweli wa Yesu Kristo. Bila shaka, ari ya kutarajia ilikuwa katika kiwango cha juu wakati huo mwanzoni mwa huduma ya Yesu. Wengine walimwona Yesu kama rabi msafiri ambaye mafundisho yake yalihatarisha hali njema ya taifa. Wengine walienda mbali zaidi kudokeza kwamba alikuwa na changamoto ya kiakili, alijidanganya, hata kudhani kuwa alitawaliwa na nguvu za yule mwovu. Bila shaka mvutano wa maswali hayo ulikuwa umeanza kutokeza siku hiyo ya Sabato asubuhi na mapema katika mji wa kwao wa Nazareti, kama Luka anavyotuambia, “hapo alipolelewa.” Akienda kwenye sinagogi, jambo la kawaida kwake kama nidhamu yake ya kiroho, alikuwa msomaji katika kusanyiko. Luka anatuambia kwamba alichukua chuo cha nabii Isaya na kusoma katika sura ya 61: “ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” Baada ya kusoma, akamrudishia mtumishi kile kitabu, akaketi. Kauli aliyoitoa baadaye ilikuwa kauli iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu mno katika mji huo, katika zama zao, na katika historia yote ya wanadamu. Yesu akawajibu, “ Leo Maandiko haya yametimia masikioni mwenu.” Kwa jibu hili, Yesu hapa anajitambulisha kuwa Mtumishi wa Yahweh aliyengojewa kwa muda mrefu, mfalme Masihi ambaye angekuja kutawala na kumiliki juu ya Ufalme wa Mungu.
ukurasa 274 2
2
Made with FlippingBook - Share PDF online