Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 4 9
M U N G U M W A N A
Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya maandiko kadhaa muhimu ambayo yanatoa muktadha wa jumla ili kuelewa tangazo kuu la Yesu juu yake mwenyewe kama Mfalme-Mtumishi (yaani, Masihi [Mpakwa-mafuta] wa Mungu): Isaya 9:6-7 - Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungumwenye nguvu, Baba wamilele, Mfalme wa amani. 7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo. Isaya 11:2-5 - Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; 3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; 4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. 5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. Isaya 42:1-4 - Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu. 2 Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. 3 Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. 4 Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake. Yesu hapa anatangaza katika mji wake wa asili kwamba, bila shaka wala utata, yeye ndiye utimilifu wa tumaini la kale la kiunabii la Mfalme Mtumishi ambaye angekuja na kuzindua upya utawala wa Mungu juu ya watu wake na uumbaji wake. Na hivyo kwa muda uliosalia wa huduma yake, angetoa uthibitisho thabiti, unaoonekana kwamba alikuwa Mfalme wa Israeli, Mtumishi wa Yehova ambaye angeitoa nafsi yake mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya dhambi za wengi (Isa. 53:1 na kuendelea). Inaweza kusemwa kwamba kunufaika kwetu na faida na baraka za Masihi kunahusiana moja kwa moja na kiwango chetu cha kuelewa na kusadiki habari zake. Kwa maneno mengine, kazi ya Mungu katika enzi hii ni kumwamini Yule ambaye Mungu alimtia mafuta na kumtuma, Yesu wa Nazareti (rej. Yoh. 6:35). Kujidhabihu kwake, kumpenda na kumwabudu, kumtii na kumtumaini ndicho kiini cha uraia katika Ufalme wa Mungu. Yesu ndiye Masihi wa kweli [Mpakwa-mafuta]
2
Made with FlippingBook - Share PDF online