Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
6 0 /
M U N G U M W A N A
d. Yesu alitangazwa kuwa “sawa na Baba,” katika uungu wake na “sawa na sisi” katika ubinadamu wake.
e. Ulihitimisha kwamba uungu na ubinadamu wa Kristo upo katika hali mbili “bila kuchanganyikana, bila mabadiliko, bila mgawanyiko, bila kutengana.”
Muungano wa Asili Mbili za Yesu
Muungano wa asili mbili za Yesu unaweza kufafanuliwa kama: “nafsi ya pili, Kristo katika hali yake kabla ya kuzaliwa alikuja na kutwaa asili ya kibinadamu na kubaki milele na Uungu usiopungua na ubinadamu wa kweli uliounganishwa katika mtu mmoja milele.” Kristo alipokuja, nafsi ilikuja, si asili pekee; alichukua asili ya ziada, asili ya kibinadamu— Hakuishi tu ndani ya mwanadamu. Matokeo ya muungano wa asili hizo mbili ni Mtu mwenye ukamilifu wa uungu ndani yake (Mungu-mtu). ~ P. P. Enns. The Moody Handbook of Theology . (Electronic ed.) Chicago: Moody Press, 1997.
D. Maana za umoja wa utu wa Yesu
1. Asili zote mbili za Yesu zimekamilika kila moja na zimeunganishwa katika utu wake.
2
2. Ufafanuzi sahihi wa asili mbili za Yesu hauwezi kuelezewa kikamilifu.
3. Yesu ndiye mpatanishi mkamilifu kati ya Mungu na mwanadamu, kwa kuwa anaweza kuwawakilisha wote wawili kikamilifu.
III. “Na Akawa Mwanadamu”: Vipengele zaidi kuhusu ubinadamu wa Yesu
A. Vipengele vya asili ya kibinadamu ya Yesu
1. Ubinadamu wake ulikuwa umekamilika : Neno alifanyika mwili (Yohana 1:14).
2. Ubinadamu wake kwa kila nanmna ulikuwa kama wetu : anashiriki kiini cha asili yetu ya kibinadamu.
a. Waebrani 2:14
Made with FlippingBook - Share PDF online