Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

6 2 /

M U N G U M W A N A

B. Makosa yanayohusiana na kutafsiri vibaya ubinadamu wa Yesu: 1 Yohana 4:2-3 - Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. 1 Timotheo 3:16 - Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katikamataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.

1. Docetism : Yesu hakuwa mwanadamu (uzushi katika Kanisa la kwanza).

2

a. Dokeo (Kigiriki, linalomaanisha “-wa kama… au -onekana kama…”)

b. Yesu alionekana tu kama mwanadamu.

c. Mungu hangeweza kuungana na mwili wa mwanadamu; Asili ya kimwili ya Yesu haikuwa halisi, ilikuwa ya kinjozi (kama roho au mzimu).

d. Dhana hii ilikanushwa moja kwa moja na maneno ya Yesu mwenyewe (Luka 24:38-43).

2. Apollinarianism : Yesu hakuwa mwanadamu kamili.

a. Askofu wa Syria katika karne ya 4

b. Yesu hangeweza kuwa na akili za kibinadamu na za kiungu.

Made with FlippingBook - Share PDF online