Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 6 5
M U N G U M W A N A
Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa na video. Somo hili linaangazia ubinadamu kamili wa Yesu wa Nazareti, na uwezo wake wa kuhurumia, kuwakilisha, na kutumika kama kielelezo cha ubinadamu mpya katika Ufalme ujao. Kuelezea uhusiano kati ya asili ya kiungu na ya kibinadamu ya Kristo kumekuwa moja ya mijadala mikuu ya kitheolojia katika historia ya Kanisa. Uwezo wetu wa kuelewa ubinadamu wa Yesu unamaana kubwa sana katika nafasi yetu ya kuwashauri wengine wanaopitia magumu na wanaohitaji kumwamini Mwokozi ambaye kwa kweli anawajali na kuelewa shida zao. Kwa hiyo uwezo wako wa kuelewa asili yake ya kibinadamu ni muhimu katika kukuwezesha kuwashawishi wengine waone kujali kwa Yesu katika nyakati zao za matatizo na uhitaji. Jibu maswali yafuatayo ukiwa na mawazo haya akilini, na ujenge hoja zako kwa kutumia Maandiko. 1. Elezea madhumuni yaliyotolewa katika somo hili kuhusu kuja kwa Yesu kama mwanadamu duniani: kufunua utukufu wa Baba kwa njia ya Umwilisho na kuwakomboa wanadamu kutoka katika nguvu, adhabu, na uwepo wa dhambi na Shetani. 2. Ni elementi gani za kiungu na za kibinadamu ambazo Yesu alizipokea kupitia kutungwa mimba na kuzaliwa kwake? Je, elementi hizi zinatusaidiaje kuelewa ukamilifu na umoja wa asili zote mbili, yaaani ile ya kiungu na ile ya kibinadamu, alizonazo? 3. Kuzaliwa kwa Yesu na bikira kuna umuhimu na uhakika gani wa kitheolojia? Ni kwa njia gani Yesu alichukua asili yetu ya kibinadamu bila kuchukua asili ya dhambi ya Adamu mwenye dhambi ? Elezea jibu lako. 4. Unestoria (nestorianism) ni nini na kwa nini ulilaaniwa katika Mitaguso ya Nikea na Konstantinopoli? 5. Ueutikiani (Eutychianism) ni nini na kwa nini ulilaaniwa katika Mitaguso ya Nikea na Konstantinopoli? 6. Tunamaanisha nini tunaposema kwamba “ubinadamu wa Yesu haukuwa na dhambi”? Na je, tunapaswa kumwelewaje Yesu kama Adamu wa Pili, yaani mwakilishi wa ubinadamu mpya mbele za Mungu? 7. Elezea uzushi wa Docetism na Apollinarianism , na kwa nini mafundisho haya yalikataliwa kama maoni mbadala katika kuuelewa ubinadamu wa Yesu Kristo. 8. Tunapata matokeo gani muhimu tunapokuwa na uwezo wa kuthibitisha kwamba Yesu wa Nazareti katika kila njia ni mwanadamu kamili kama sisi tulivyo, katika suala la uwezo wake wa kutujali, kutuwakilisha mbele za Mungu, na kutumika kama kielelezo cha ubinadamu wetu wenye utukufu katika ulimwengu ujao?
Sehemu ya 1
Maswali kwa wanafunzi na majibu
ukurasa 277 4
ukurasa 277 5
2
Made with FlippingBook - Share PDF online