Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

6 4 /

M U N G U M W A N A

Hitimisho

» Katika muungano wa asili mbili za Kristo, asili ya kiungu na ya kibinadamu ya Yesu zimeunganishwa kikamilifu katika mtu mmoja: Yesu ni mwanadamu kamili, kwa kila namna kama sisi, lakini hana dhambi . » Kanuni ya Imani ya Nikea inathibitisha mafundisho ya Maandiko Matakatifu kuhusu Uungu kamili na ubinadamu kamili wa Yesu Kristo. » Yesu, huko Nazareti, alichukuliwa mimba kwa RohoMtakatifu na kuzaliwa na Bikira Maria. Asili zake mbili, yaani ile ya kiungu na ya kibinadamu, zimekamilika na zimeunganishwa kikamilifu katika mtu mmoja. Mkanganyiko wa kenosis unahusu ufasiri wa Wafilipi 2:7, “(Yeye) alijifanya kuwa hana utukufu” *[tafsiri sisisi ingesomeka] “alijifanya mtupu [Gk. ekenosen] Mwenyewe.” Swali muhimu ni: Kristo alijiondoa nini? Wanatheolojia huria wanadai kwamba Kristo alijiondoa uungu wake, lakini ni dhahiri kutokana na maisha na huduma yake kwamba hakufanya hivyo, kwa maana uungu wake ulidhihirishwa mara nyingi. Mambo mawili makubwa yanaweza kuonyeshwa hapa: (1) “Kristo alisalimisha tu utendaji huru wa baadhi ya sifa zake za shirikishi au za kimahusiano. Hakusalimisha kwa maana yoyote sifa zake za binafsi, yaani zisizohusiana na uumbaji wake; Daima alikuwa mtakatifu kabisa, mwenye haki, mwenye rehema, mkweli, na mwaminifu.”30 Usemi huu unastahili na unatoa suluhisho kwa vifungu vinavyoleta shida kuelewa kama vile Mathayo 24:36. Neno kuu katika ufafanuzi huu lingekuwa “kujitegemea” kwa sababu Yesu alifunua mara nyingi sifa zake shirikishi. (2) Kristo alichukua asili ya ziada. Muktadha wa Wafilipi 2:7 unatoa suluhisho bora kwa mkanganyiko wa kenosis. Kujifanya mtupu hakukuwa kwa kuondoa bali kwa kuongeza. Vishazi vinne vifuatavyo (Flp. 2:7–8) vinaelezea dhana hii ya kujifanya mtupu: “(a) akatwaa namna ya mtumwa, na (b) akawa ana mfano wa wanadamu. Tena, (c) alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, (d) alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti.” “Kujifanya mtupu” kwa Kristo kulikuwa ni kuchukua asili ya ziada, asili ya kibinadamu pamoja na mipaka yake. Uungu wake haukusalimishwa kamwe [msisitizo wangu]. ~ P. P. Enns. Moody Handbook of Theology . Chicago: Moody Press, 1997. Kenosis (Kujifanya mtupu) kwa Kristo: Alijiondoa Nini?

2

*Katika mabano [ ] ni nyongeza ya mtafsiri kwa ufafanuzi zaidi.

Made with FlippingBook - Share PDF online