Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

/ 7 1

M U N G U M W A N A

e. Mafundisho yake yalionyesha uthibitisho wa maadili ya ufalme wa Mungu hapa na sasa, kwa mfano, Mahubiri ya Mlimani (Mt. 5-7). (1) Upendo kama amri kuu na utimilifu wa kanuni za maadili za Torati (Mt 22:34-40). (2) Yeye mwenyewe kama mhusika anayezungumzwa na Musa, Zaburi na Manabii (yaani, Agano la Kale kwa ujumla wake; rej. Yoh. 5:39-40; Lk 24:27, 44-48).

f. Tabia yake inadhihirisha utukufu wa fahari ya Baba mwenyewe pamoja na haki ya ufalme wake (Yoh. 1:14; Mt. 5:17-18).

2

B. Tafsiri za kitheolojia za Yesu kama Mtangaza Ufalme wa Mungu

1. Yesu ndiye utimilifu wa unabii wa Agano la Kale kuhusu ujio wa Bwana na Masihi (Mdo 2:34-36).

2. Kupitia ujio wa Yesu mara ya kwanza, Ufalme wa Mungu umekuja na kuzinduliwa. Ingawa hautakamilishwa hadi Ujio wake wa Mara ya Pili, Yesu amewahamisha wale wanaoamwamini katika Ufalme wa Mwana wa pendo lake (Kol. 1:13; 1 Yoh. 3:8).

3. Utume wa Yesu duniani ulikuwa onyesho na uthibitisho wa utawala wa Mungu katika eneo hili, kumshinda shetani na kurejesha uumbaji chini ya utawala wa Mungu (1 Yoh. 3:8).

Anaitwa Mtumishi Wake na Mungu wa vitu vyote, na Israeli, na Nuru ya Mataifa. ~ Origen (c. 228, E), 9.314. Ibid. uk. 370.

III. Yesu ni Mtumishi wa Yehova Atesekaye.

A. Taswira ya Kibiblia ya Mtumishi wa Yehova

Made with FlippingBook - Share PDF online