Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
7 0 /
M U N G U M W A N A
c. Utaratibu wa kijamii utabadilishwa: Ukandamizaji wa Mataifa utakoma.
d. Uumbaji wote utabadilishwa.
5. Alipokuja mara ya kwanza, Yesu alijitangaza mwenyewe kama uwepo wa Ufalme wa Mungu katika nafsi yake.
a. Alijitambulisha kuwa ndiye Masihi aliyeahidiwa wa Ufalme ambao ulikuwa umetokea wakati huo, Mk 1:14-15.
2
b. Jina lake la cheo lililotumika mara nyingi zaidi ambalo alijiita lilikuwa “Mwana wa Adamu,” dokezo la mfalme ajaye wa unabii wa Danieli (Dan. 7:13-14).
c. Alitumia mamlaka juu ya Shetani na wafuasi wake kupitia huduma yake ya kutoa pepo na ukombozi.
(1) Luka 11:17-23 (2) Luka 10:17-20 (3) Matendo 10:36-38
d. Alitoa ishara za kuja kwa Ufalme na mwisho dhahiri wa nguvu za laana kupitia uponyaji na miujiza yake. (1) Kulisha watu 5,000 (rej. Marko 6:30-44) (2) Alifungua macho ya vipofu (Yoh 9:1-7). (3) Aliamuru pepo za dhoruba na mawimbi (Mt. 8:23-27). (4) Aliponya viwete, waliopooza, na wagonjwa (k.m., Marko 2:1-12). (5) Alifufua wafu (Yohana 11).
Made with FlippingBook - Share PDF online