Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
7 4 /
M U N G U M W A N A
Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kupitia ulichojifunza katika sehemu ya pili ya video. Katika kila mojawapo ya mada hizi tatu za kibiblia (picha, taswira), Yesu anajidhihirisha kuwa ndiye Masihi wa Israeli aliyengojewa kwa muda mrefu. Katika ubatizo wake alijihusianisha na wenye dhambi aliokuja kuwakomboa. Katika tangazo lake la Ufalme, alizindua utawala wa Mungu na kuthibitisha haki ya Mungu ya kutawala juu ya uumbaji. Katika kutimiza kwake unabii wa Agano la Kale, alionyesha waziwazi ishara za Yule aliyepakwa mafuta na Mungu kutoa uhai wake kuwa fidia kwa ajili ya wengi. Uelewa wa taswira hizi ni msingi wa huduma ya mijini, hasa kwa vile jamii za watu waishio mijini zina haja sana na Yule anayeelewa maumivu yao, anayetangaza Habari Njema ya amani na upatanisho, na ambaye anaweza kurejesha mahusiano ambayo yamevunjika kati yao na Mungu na baina yao katika jamii. Jibu maswali yafuatayo ukiwa na ufahamu huu muhimu akilini unapojaribu kuelewa kwa ufasaha kweli zinaounga mkono mada hizi kuu za kibiblia. 1. Yohana Mbatizaji alikuwa na jukumu gani katika habari za Yesu wa Nazareti na kutangazwa kwa Masihi? 2. Je, tunapaswa kuelewaje maana ya Yesu kubatizwa na Yohana, hasa tukizingatia kwamba Yesu hakuwahi kutenda dhambi—kwa nini Yesu alishiriki ubatizo wa toba? Elezea jibu lako. 3. Ni kwa jinsi gani ubatizo wa Yesu unaweza kuhusiana na jukumu lake kwetu kama kuhani mkuu, yaani, kama mtu ambaye lazima aweze kuchukuliana na mahitaji na udhaifu wa watu (rej. Ebr. 4:14-15 - Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi)? 4. Katika hadithi ya Mungu, Wayahudi wa siku za Yesu walielewa udhihirisho walioutarajia wa utawala wa Mungu ungetukiaje? Mafundisho na huduma ya Yesu vilionyeshaje uelewa mpya wa ratiba na udhihirisho wa Ufalme kwa njia ya Yeye mwenyewe ? 5. Yesu alionyeshaje kupitia miujiza na uponyaji kwamba Ufalme wa Mungu uliotabiriwa kwa muda mrefu ulikuwa umekuja kupitia maisha na huduma yake? Mafundisho yake yalionyeshaje uhalisia wa uwepo wa Ufalme wa Mungu sasa kupitia maishani yake? 6. Kuna uhusiano gani kati ya kuzinduliwa kwa kwanza kwa Ufalme na Yesu na Kuja kwake Mara ya Pili? Elezea jibu lako. 7. Yesu alitangazaje utambulisho wake katika tangazo lake la hadharani katika mji wa kwao Nazareti? Alijitambulisha kama nani? Kwa nini hili ni la muhimu katika kulielewa jukumu la Yesu kama Masihi?
Sehemu ya 2
Maswali kwa wanafunzi na majibu
2
Made with FlippingBook - Share PDF online