Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide
/ 7 5
M U N G U M W A N A
8. Je, Agano la Kale (k.m. Isaya 53) linaelezeaje huduma ya Mtumishi wa Yahwe kama dhabihu mbadala kwa ajili ya dhambi za watu? Kifo cha Yesu kilitimizaje unabii huo muhimu? 9. Kwa nini tunaweza kuwa na uhakika kwamba ikiwa Yesu kweli ni Mtumishi wa Yehova Atesekaye, atarudi na kukamilisha kazi aliyoianza kupitia kufanyika kwake mwili, kifo na ufufuo wake?
Umuhimu wa Kanuni ya Imani ya Nikea katika mabishano ya Kikristolojia
Kanuni ya Imani ya Nikea, ambayo inatumiwa katika ibada leo, imetokana na Mtaguso wa Konstantinopoli mnamo mwaka 381. Kanuni za Imani zote zinazotumia maneno “mwenye asili (uhalisia, kiini) moja na Baba” zilichukuliwa kuwa za Nikea. Mtaguso wa Konstantinopoli pia uliondoa laana kutoka kwenye Kanuni ya Imani ya 325 na kuongeza kauli inayothibitisha uungu wa Roho Mtakatifu pamoja na Kanisa moja takatifu katoliki, msamaha wa dhambi, na ufufuo wa wafu. Mtaguso wa Nikea, katika kuthibitisha kwamba Yesu Kristo alikuwa Mungu kweli, ulizua swali la ubinadamu wa Kristo, ambalo lilizaa swali la fundisho la nafsi ya Kristo. Kanisa la karne ya 5, katika jitihada ya kitheolojia ya ajabu ya kikatoliki, lilifafanua ufahamu wake wa nafsi ya Yesu Kristo kwenye Mtaguso wa Kalkedon (431) ambamo lilithibitisha kwamba Yesu Kristo ni Mungu kweli na mwanadamu ndani ya mtu mmoja (mhusika mmoja). ~ John H. Leith. “Creeds.” The Anchor Bible Dictionary . D. N. Freedman, ed. (Vol. 1). (electronic ed.). New York: Doubleday Publishers, 1996. p. 1205. Somo hili linaangazia mafundisho muhimu kuhusu Kristo katika ubinadamu wake na pia utajiri wa maisha na huduma yake kama Masihi aliyeahidiwa kama alivyodhihirisha katika ubatizo wake, huduma ya Ufalme, na kujihusianisha na taswira ya Mtumishi wa Yehova Atesekaye. Dhana muhimu zilizomo katika somo hili ni muhimu kwa viongozi wa mijini kuelewa na kutumia sio tu wanapomfuata Bwana katika ufuasi wao binafsi, lakini pia wanapowaongoza wengine kuufikia ukomavu. Katika orodha hapa chini ni baadhi ya dhana na kweli hizi muhimu. ³ Kusudi kuu la kuja kwa Yesu duniani lilikuwa kutufunulia utukufu wa Mungu Baba katika nafsi yake, na pia kuwakomboa wanadamu kutoka katika adhabu na nguvu za dhambi na Shetani.
2
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
ukurasa 278 6
Made with FlippingBook - Share PDF online