Mungu Mwana – Mwongozo wa Mkufunzi: Capstone Module 10 Swahili Mentor Guide

7 8 /

M U N G U M W A N A

ufufuo wake, kupaa kwake, na kurudi kwake (rej. Rum. 8:29; Gal. 4:10 na kuendelea; Flp. 3:20-21; 2 Kor. 3:18; 1 Yoh. 3:1-2; Rum. 6:1-11, nk). Ni kwa jinsi gani fundisho la Yesu kama Mtumishi wa Yehova Atesekaye linaweza kutusaidia kuelewa kusudi la Mungu la kutufananisha na mfano wake, tukishiriki mateso na kifo chake ili kushiriki katika kuinuliwa na utukufu wake (1 Pet. 2:21-25; Rum. 8:16-18)?

Amewahi kupitia hali hiyo!

MIFANO

Katika kuishauri familia iliyofiwa na mtoto mdogo hivi majuzi, wewe mchungaji unaitwa ili kuwapa maneno ya faraja. Kati ya mawazo yote ambayo yamewasababishia uchungu mkubwa, wazo moja linaloendelea ni hofu waliyo nayo juu ya kifo. Wao ni Wakristo, wanampenda Bwana na ni washirika waaminifu wa kanisa thabiti, la kibiblia, lenye nia ya umisheni, lakini kuondoka kwa binti/dada yao kumeifadhaisha mno familia. Wanataka kuamini kwamba Mungu anaelewa na kwamba mtoto wao mdogo Sara yuko katika mikono yake, lakini katika siku zao za majonzi makubwa, wanaelekea kulemewa na huzuni na maumivu. Ni kwa jinsi gani mafundisho ya ubinadamu wa Yesu yanaweza kukuwezesha kuwasaidia kukabiliana na tukio la kumpoteza mtoto wao mdogo? Kujua kwamba Yesu alikufa kunaweza kukusaidiaje kuwafariji kwa kufiwa na Sara? Je, Paulo anaunganishaje ujuzi wake wa Kristo katika ushauri wake kwa Wathesalonike juu ya somo hili hili (yaani, 1 Thes. 4:13-17)? Ili kufanya kazi njema ya theolojia ni lazima tuwe tayari kutumia mawazo na akili zetu kuelewa kile ambacho Mungu ametoa kwa ajili yetu. Katika majadiliano kuhusu asili ya makusudi ya Mungu na Umwilisho, baadhi ya wanafunzi wa juu wa seminari katika somo la Kristolojia walizua swali la umuhimu na kutoepukika kwa Umwilisho (Mungu kuvaa mwili). Waliuliza, ni kwa namna gani, kama ipo, lilikuwa ni jambo lisiloepukika kwelikweli? Kwa maneno mengine, je, Yesu wa Nazareti angezaliwa endapo Adamu asingefanya dhambi, na wanadamu wasingehitaji Mwokozi? Mwanafunzi mmoja anaamini kwamba mawazo hayo yote yana thamani ndogo au hayana thamani kabisa, kwa kuwa mambo ya siri ni ya Mungu na mambo yaliyofunuliwa ni yetu (Kum. 29:29). Mwingine anaamini kwamba mawazo hayo yana manufaa, akitolea mfano jitihada za malaika pamoja na manabii za kutamani kuelewa nia na makusudi ya Mungu yaliyoandikwa katika Maandiko (1 Pet. 1:10-12). Unasemaje juu ya hili? Angekuja?

1

ukurasa 280  7

2

2

Made with FlippingBook - Share PDF online